Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Sample

Hushai akawaambia ... pelekeni habari upesi, kamwambieni Daudi ya kwamba, Usilale usiku huu karibu na vivuko vya jangwani; bali usikose kuvuka; asije akamezwa mfalme (m.15-16). Mpango wa Daudi kuwa Hushai atasaidia kuyavunja mashauri ya Ahithofeli ulifanikiwa (habari ya mpango inapatikana katika 15:34-37). Kutokana na uchovu, Daudi alikuwa hajavuka mto. Lakini sasa alipata muda wa kukimbia na kujiandaa! Maana alipata onyo la Hushai, na Absalomu alifuata shauri la Hushai! Linganisha m.27-29 na Zaburi 23: Ikawa, Daudi alipofika Mahanaimu, Shobi, mwana wa Nahashi wa Raba, wa wana wa Amoni, na Makiri, mwana wa Amieli wa Lo-debari, na Barzilai, Mgileadi wa Rogelimu, wakaleta magodoro, na mabakuli, na vyungu, na ngano, na shayiri, na unga, na bisi, na kunde, na dengu, na asali, na siagi, na kondoo, na samli ya ng'ombe, wapate kula Daudi na watu waliokuwa pamoja naye; kwani walisema, Watu hao waona njaa, tena wamechoka, nao wana kiu huku nyikani. Katika Zab 23:5 Daudi anashuhudia, Waandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu.
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Related Plans

Returning Home: A Journey of Grace Through the Parable of the Prodigal Son

Homesick for Heaven

Breath & Blueprint: Your Creative Awakening

Judges | Chapter Summaries + Study Questions

Stormproof

Let Us Pray

Ruth | Chapter Summaries + Study Questions

Faith in Hard Times

Unapologetically Sold Out: 7 Days of Prayers for Millennials to Live Whole-Heartedly Committed to Jesus Christ
