YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?Sample

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

DAY 4 OF 7

Ni ya watu wote. Roho mtakatifu haupatikani katika njia za ki-karata, kumaanisha ni watu wachache tu wanaopata tuzo la Roho. Sio mchezo wa karata. Hakuna washindwa au washindani. Walioitwa na Mungu wanapewa uwezo wake. Nguvu na uwezo wa Mungu unatosha watu wote duniani. Hakuna anayewachwa nyuma au kupokea mabakisho. Usijitenge naye kwani umeshakubaliwa. Maandishi ya Bibilia yanaeleza kwa uwazi. Ubatizo katika Roho Mtakatifu haujatolewa kwa wale wanao julikana kama “wapendwa wake Mungu” Hapana. Mungu hana “wapendwa binafsi” kwani sisi wote duniani ni wapendwa wake. Katika siku ya Pentekoste, wake na waume 120 waliokuwa katika chumba cha juu kule Yerusalemu, na tunasoma katika Matendo ya Mitume 2:3 na 4 “Pakatokea kitu kama ndimi za moto ambao uligawanyika ukakaa juu ya kila mmoja wao. 4Wote walijazwa Roho Mtakatifu wakaamza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kusema.” Kitendo hiki halikuwa cha kibahati au Karata! “Kila Mmoja’ wa hao 120 walijazwa na Roho Mtakatifu. Hakukuwa na ubaguzi wa kizazi au umri, au ukoo ama hadhi katika maisha. Inawezekana vichwa vilihesabiwa mbinguni kwani ndimi za moto zilishuka vichwani vya kila mmoja wao. Yaani kama ulikuwa na kichwa, ulimi wa moto ulitumwa kwako. Uko katika hesabu zake mwenyezi Mungu. Matendo ya Mitume 1:8, “ Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.” Tafakari haya, kichwa chako kinakuwa kikalio cha moto wa Roho Mtakatifu. Anasimamia hapo, bila kutoka tena. Kila mmoja wa wafuasi 120 waliokuwa katika chumba cha Juu siku ya Pentekoste walipokea ubatizo wa Roho Mtakatifu . Hakuna mmoja aliachwa au kusahaulika. Yaani, sio wafuasi 12 waliokuwa karibu na Yesu, ilhali, wengine wasiojulikana walipata Roho Mataktifu. Hawakuwa watu wa umaarufu, lakini walikuwa waaminifu. Walijitolea kuwa katika chumba cha juu na kusubiri ahadi yake Yesu. Roho Mtakatifu ulishuka katika ndimi za moto na kusimamia vichwa vyao wote – ndimi za moto 120, tuzo kwa waaminifu 120. Ukijitolea na kungoja ahadi zake Yesu, utapata moto na uwezo wa kutimiza utumishi wako.

Scripture

Day 3Day 5

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy