YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

DAY 17 OF 31

Wakajikwaa kwake (m.3). Yesu alikuwa amefika nyumbani Nazareti (ni maana ya “nchi ya kwao” katika m.1). Watu wa nyumbani walikuwa wanashangaa. Kwa upande mmoja walikubali kuwa mafundisho yake na matendo yake ni ya pekee sana, maana waliposikia [aliyowafundisha] wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? (m.2). Kwa upande mwingine walijua Yesu ni seremala tu wala si mwalimu wa dini (mwanatheolojia) aliyepitia mafunzo kwa walimu wao wa dini ya Kiyahudi (m.3). Huenda walifikiri anayafanya kwa nguvu ya Shetani? Ugumu wao wa kupokea ulimfanya Yesu kuwaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake. Neno hili la Yesu katika m.4 lituonye kwamba tusijikwae, Mungu akiamua kumjalia mtu wa kwetu kwa njia ya pekee!

Scripture