Soma Biblia Kila Siku 10/2020Sample

Kwa kutumia Neno la Mungu katika kujipima tunatambua dhahiri kwamba hatuna lolote la kujivuna. Usihofu juu ya mafanikio ya watu wengine. Badala yake endelea kujiuliza, Je, ninaonekanaje mbele ya Mungu? Maisha yangu yanalinganaje na Yesu Kristo? Yesu Kristo ndiye ainuliwe, na sisi tushuke (ling. Yohana Mbatizaji alivyojitambulisha mbele ya Yesu: Mimi sistahili kuilegeza gifamu ya viatu vyake; Lk 3:16). Ni yeye Yesu Kristo wa kutuinua. Fungua milango ya kumjulisha Kristo na si wewe mwenyewe. Ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi(Yer 9:24). Paulo anaandika vivyo hivyo: Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana(1 Kor 1:31).
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More