YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 06/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

DAY 3 OF 30

Ni pendo la namna gani alilotupa Baba (m.1). Mungu hakuuhakikisha upendo wake kwa neno tu, hata alitupa upendo wake kwa njia ya Kristo. Kumbuka mfano wa Mwana mpotevu, jinsi baba yake alivyompa upendo wake. Kuna habari tunazozijua, na kuna habari tusizozijua (m.2). Hizo za mwisho zitaonekana Yesu atakaporudi. Tutamwona katika utukufu wake. Hapa duniani tulimwona kama binadamu. Alikuwa kama sisi ili sisi tupate kumwona kama yeye alivyo katika utukufu wake. Zingatia m.3: Kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.Neno hili kuhusu kujitakasa si amri, bali ni matokeo ya yaliyotangulia kutendeka. Hivyo ni hali halisi ...kama yeye [Yesu]alivyomtakatifu.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More