YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 04/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

DAY 2 OF 30

Palipo na mauti hueleza kuwa ghadhabu imepitia na dhambi imepatilizwa; maana mshahara wa dhambi ni mauti. Saa ya kufa kwa Yesu msalabani, Mungu alizuia msaada wake kwa mwana wake mpendwa, ili afe na kulipa gharama kamili ya dhambi zetu. Zaidi ya kulipa deni la dhambi, pazia la hekalu lililotenga watu na PATAKATIFU PA PATAKATIFU, lilipasuka kuonyesha kuwa sasa twaweza kwenda mbele za Mungu bila kuhitaji tena kuhani wa kutuombea. Sote tunawiwa kumshukuru Mungu kwa wokovu mkuu jinsi hii.