YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 8Sample

Soma Biblia Kila Siku 8

DAY 27 OF 31

Kabla Yesu hajafa alisema: Imekwisha (m.30). Kwa tafsiri nyingine alisema: Yametimia. Imekwisha nini? Kazi yake ya wokovu imekwisha: Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ... Hakuna aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe ... Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu(Yn 10:17-18). Kitu gani kimetimia? Yametimia Maandiko yasemayo kwamba ndivyo alivyotakiwa Masihi kuteseka kwanza kabla hajatukuzwa na kupewa mamlaka yote Mbinguni na duniani (m.24: Askari wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, na vazi langu wakalipigia kura. m.28: Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.Na m.36-37: Hayo yalitukia ili andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena andiko lingine lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma. Linganisha habari hizo na Yesu anayosema katika Yn 5:39: Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia).

Scripture