Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!Sample

“Ubatizo wa Maji: Tamko kwa Umma la Maisha Yaliyobadilishwa”
Ubatizo wa maji ni njia muhimu ya kuutangazia umma juu ya wokovu wako. Ubatizo wa Maji unasheherekea mwisho wa jinsi ya zamani ya maisha na mwanzo wa aina mpya ya maisha. Yesu alifundisha umuhimu wa ubatizo wa maji kwa wanafunzi wake kabla tu ya kupaa kwake kwenda mbinguni baada ya kufufuka. Alisema,
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.” Mathayo 28:19
Agano Jipya lote, lina simulizi nyingi za waamini kubatizwa. Ubatizo wa maji unaonyesha ishara muhimu kwa anayebatizwa, na wao wanaoangalia. Ubatizo wa maji unaonyesha wazi kwa watu: mwisho wa maisha yako ya zamani kwa kuzamishwa kwenye maji, na mwanzo wa maisha mapya katika Kristo kwa kutoka ndani ya maji uliyesafishwa, uliyetakaswa na kiumbe kipya katika Mungu.
Luka 3:3 inawakilisha ubatizo wa maji kama “ubatizo wa toba,” na kusisitiza umuhimu wa kutangaza mbele ya watu kwamba tumebadilika kutoka maisha yetu ya zamani na dhambi. Ingawa ubatizo wa maji hautuokoi wala kufunika dhambi zetu, unawakilisha sehemu muhimu ya maisha yetu ya Ukristo – tangazo kwamba wewe ni kiumbe kipya, maisha yaliyo badilishwa! Kama kuna mtu ambaye hakupaswa kutoa tamko hili, basi angekuwa ni Yesu, ambaye hakuishi maisha ya dhambi hapa duniani. Luka 3:21 inasema,
“Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, Yesu naye amebatizwa,” Luka 3:21
Yesu alibatizwa ili tuweze kufuata mfano wake. Ubatizo wa maji ni muhimu. Kama hujabatizwa katika maji, unapaswa kufikiria kufanya jambo hilo kuwa ni kipaumbele. Biblia inatuagiza sisi kutoa tamko la wazi la wokovu wetu, na mengi ya makanisa yanayoamini juu ya Biblia yanatoa fursa nyingi juu ya kupata ubatizo wa maji. Kufuata mfano wa Yesu siku zote ni kujiweka katika ushindi. Mungu atakubariki sana na kukumbuka kwa uamnifu wako na utii Kwake!
Scripture
About this Plan

Maamuzi mengi katika maisha huwa na athari fulani. Hata hivyo, ni uamuzi mmoja tu ndio muhimu zaidi. Kama unatafuta maelekezo rahisi ya kukuwezesha kuelewa kwa undani juu ya uamuzi huu wa ajabu – zawadi ya bure ya wokovu ya Mungu - basi anzia hapa. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo katika Kukua na Kusudi ” kilichoandikwa na David J. Swandt
More
Related Plans

HEAL BOLDLY: Healing Is Holy Work - a 5-Day Devotional Journey for Women Ready to Heal, Grow, and Rise

Gems of Motherhood~ Letters to a Mama: 20ish Things I Wish I Knew Before Becoming a Mom

Consciousness of God's Presence

Whiskers & Prayers: Devotionals for Cat Lovers

The Unworthy Parent: God’s Grace in Your Gaps

Note to Self: Helpful Reminders for Healthier Relationships

Wellness Wahala: Faith, Fire, and Favor on Diplomatic Duty

Start Strong: 7 Prayers for Bold New Beginnings

LIVE BOLDLY: Embracing the Abundant Life You Were Born for - Embracing the Abundant Life You Were Born For
