YouVersion Logo
Search Icon

Tito UTANGULIZI

UTANGULIZI
Msomaji atagundua hapa kama vile katika 1 na 2 Timotheo kwamba ingawa barua imeandikwa kwa mtu binafsi, ujumbe wa barua hii sio kwa ajili ya mtu mmoja. Matatizo yanayoshughulikiwa hapa ni matatizo ambayo yanakabiliwa na Kanisa lote la wakati ule na sasa. Kwa mfano tatizo la kuweka mpango wa kufaa katika jumuiya ya Wakristo au juu ya sifa zinazotakiwa kwa viongozi wake.
Kuhusu Tito ambaye barua hii inachukua jina lake, tunajua machache sana, maana hata Luka hamtaji katika kitabu cha Matendo ya Mtume. Katika barua kwa Wagalatia 2:3, tunajua Tito alizaliwa katika jamaa ya Kigiriki, akawa Mkristo. Alikuwa mmoja wa wahudumu wenzake Paulo na alikuwa na mengi ya kufanya katika kuipatanisha jumuiya ya Wakristo wa Korintho na Paulo (2Kor 7:6-16). Wakati Paulo alipoandika barua hii, alikuwa amemtuma Tito kisiwani Krete ambako alimwagiza aongoze shughuli za kuliweka kanisa la huko katika mpango unaofaa (1:5).
Barua hii ilipelekwa kwa Tito wakati alipokuwa Krete, na inafanana kwa kiasi kikubwa na 1 Timotheo kuhusu mambo yaliyomo na hata muundo wake wa kimaandishi. Baada ya maneno ya kujitambulisha na salamu (1:1-4), Paulo anamfundisha mwanafunzi wake kuhusu sifa zinazotakiwa katika waumini hasa wale walioitwa kuwa na majukumu katika Kanisa. Vilevile anamhimiza awakemee na kuwaonya watu walio wakaidi na wanaowapotosha wengine na wanaoshikilia hadithi tupu za Kiyahudi (1:10,14). Kwa kusema hivyo Paulo anagusia lile jambo la waalimu wa uongo ambao kwa mafundisho yao walivuruga jumuiya nzima (1:11) na pia desturi fulanifulani zisizofaa (1:5-11). Ingawa anatumia maneno makali kuhusu Wakrete (1:12-16), anamshauri Tito juu ya mambo ya kichungaji na kumtia moyo ayatekeleze daima kwa mfano mwema mbele ya waumini wote bila kubagua umri, jinsia au cheo na hali ya mtu katika jamii (2:1–3:2).
Mafundisho juu ya uadilifu na wokovu kwa neema ya Mungu na kazi ya Roho Mtakatifu (2:11,14 na 3:4-7) ni msingi wa mashauri ya Paulo ili Tito na yanafaa kwa ajili ya kumfanya Tito awe imara katika kuongoza na kuimarisha Kanisa kiroho (3:1-3,8-11). Barua inamalizia na maagizo ya binafsi na baraka (3:12-15).

Currently Selected:

Tito UTANGULIZI: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy