YouVersion Logo
Search Icon

Waroma UTANGULIZI

UTANGULIZI
Huenda Barua hii ya Paulo kwa Waroma iliandikwa huko Korintho, mnamo mwaka wa 55 B.K. wakati wa safari yake ya tatu ya kuhubiri Habari Njema. Barua hii iliandikwa na Paulo kutayarisha safari yake huko Roma (1:7) kuwaona Wakristo wa mji huo ambao waliwafahamu Priska na Akula (taz 16:3-5). Paulo aliandika kuwaelezea jinsi alivyoielewa imani ya Kikristo na matokeo yake katika maisha ya Wakristo: “Habari Njema ni nguvu ya Mungu ya kuwaokoa wote wanaoamini, Wayahudi kwanza, na watu wasio Wayahudi pia” (1:16), na kwamba “… Habari Njema inaonesha wazi jinsi Mungu anavyowakubali watu kuwa waadilifu; jambo hili hufanyika kwa imani, tangu mwanzo mpaka mwisho” (1:17). Uhusiano huo Paulo anauendeleza katika sehemu zifuatazo za barua hiyo.
Sura 1–4 Paulo anatamka wazi: Hakuna mtu yoyote, awe Myahudi au sio, anayeweza kujifanya kuwa sawa mbele ya Mungu. Ama kweli kila mtu amevunja sheria ya Mungu. Mungu naye aweza kuwaadhibu watu, lakini anapendelea zaidi kuwaacha. Kwa kumwamini Yesu Kristo lakini, watu wanaweza kukubalika kwa Mungu na kutakaswa maovu yao kwa njia ya Roho wake Mungu. Sura 5–8 Paulo anaonesha maana na madhumuni ya sheria na nguvu na uwezo wa Roho wa Mungu.
Sura 9–11 Paulo anaandika juu ya suala la nafasi ya Wayahudi na watu wasiomjua Mungu (wapagani), katika mpango wa Mungu. Watu wa mataifa mengine wanahubiriwa Habari Njema, maana kwake Yesu Kristo binadamu wote wanaweza kupewa fadhili na neema ya Mungu.
Sura 12–16 Paulo anaonesha jinsi ipasavyo kuishi maisha ya Kikristo kama jibu kwa vitendo juu ya yote aliyotenda Yesu kwa ajili yetu. Mwishoni mwa barua mna salamu na heri za Paulo kwa watu binafsi.

Currently Selected:

Waroma UTANGULIZI: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy