YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 65

65
Wimbo wa shukrani
(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi: Wimbo)
1Wastahili sifa, ee Mungu, huko Siyoni,
watu watakutimizia wewe ahadi zao,
2maana wewe wajibu sala zetu.
Binadamu wote watakujia wewe.
3Tunapolemewa na makosa yetu,
wewe mwenyewe watusamehe.
4Heri wale unaowachagua na kuwaleta karibu,
waishi katika maskani yako.
Sisi tutatoshelezwa na mema ya nyumba yako;
mema ya hekalu lako takatifu.
5Kwa matendo yako makuu watuitikia na kutuokoa,
ewe Mungu wa wokovu wetu;
wewe ndiwe tumaini la viumbe vyote,
duniani kote na mbali baharini.
6Kwa nguvu yako uliisimika milima mahali pake.
Wewe una nguvu mno!
7Watuliza mshindo wa bahari na wa mawimbi yake,
wakomesha ghasia za watu.
8Ulimwengu wote washangazwa na matendo yako.
Wasababisha furaha kila mahali,
toka mashariki hata magharibi.
9Wewe waitunza nchi kwa kuinyeshea mvua,
waijalia rutuba na kuistawisha;
mto wako umejaa maji tele,
waifanikisha nchi na kuipatia mavuno.
Hivi ndivyo uitengenezavyo nchi:
10Mashamba wayanyeshea mvua kwa wingi,
na kuyalowanisha kwa maji;
ardhi wailainisha kwa manyunyu,
na kuibariki mimea ichipue.
11Wautunukia mwaka wote mema yako,
kila ulipopitia pamejaa fanaka.
12Mbuga za majani zimejaa mifugo,
milima nayo imejaa furaha.
13Malisho yamejaa kondoo,
mabonde yamefunikwa kwa ngano.
Kila kitu kinashangilia kwa furaha.

Currently Selected:

Zaburi 65: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy