YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 120

120
Kuomba msaada
(Wimbo wa Kwenda Juu#120:1 Zaburi hizi huenda ziliimbwa wakati wa kuhiji au kutoka Yerusalemu ambamo kilimani kulikuwa na lile hekalu.)
1Katika taabu yangu nilimwita Mwenyezi-Mungu,
naye akanijibu.
2Uniokoe ee Mwenyezi-Mungu,
na watu wadanganyifu na waongo.
3Enyi watu wadanganyifu, mtapewa kitu gani?
Mtaadhibiwa namna gani?
4Kwa mishale mikali ya askari,
kwa makaa ya moto mkali!
5Ole wangu kwamba naishi kama mgeni huko Mesheki;
naishi kama mgeni katika mahema ya Kedari.#120:5 watu wa Mesheki na Kedari walidhaniwa kuwa wabaya sana.
6Nimeishi muda mrefu mno
kati ya watu wanaochukia amani!
7Wakati ninaposema nataka amani,
wao wanataka tu vita.

Currently Selected:

Zaburi 120: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy