YouVersion Logo
Search Icon

Nehemia UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu hiki kinaendeleza masimulizi ya kitabu kilichotangulia, yaani Kitabu cha Ezra. Nehemia aliishi wakati wa Ezra na alikuwa Afisa maarufu katika utawala wa Artashasta, mfalme wa Persia. Nehemia alipata kibali kutoka kwa mkuu wake arudi Yerusalemu ajishughulishe na urekebishaji wa maisha ya siasa, uchumi na jamii (sura 1:1–2:10). Mara alipowasili huko, ingawa alikumbana na upinzani kutoka kwa maadui fulani, aliungwa mkono na baadhi ya wananchi wenzake wakajenga kuta za mji wa Yerusalemu (sura 2:11–7:72). Nehemia na Ezra walikuwako wakati wa mkutano mkubwa wa kidini ambamo Ezra alihutubu juu ya sheria ya Mungu.
Watu walirudia tena maagano yao kwa Mungu (sura 8:1–10:40). Baada ya kutoa mawaidha mbalimbali yaliyohusu hasa mambo ya siasa, Nehemia alisimamia kuwekwa wakfu kwa kuta zilizojengwa upya (11:11–12:43), kisha akaendelea na mambo mengine ya kurekebisha mfumo wa dini (sura 12:44–13:31).

Currently Selected:

Nehemia UTANGULIZI: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy