YouVersion Logo
Search Icon

Mika UTANGULIZI

UTANGULIZI
Mika alihubiri karibu nyakati zilezile za nabii Isaya yapata miaka 750 – 700 K.K. na mahubiri yake yalikuwa kwa wakazi wa utawala wa kusini, yaani Yuda. Labda alikuwa mwanafunzi wa Isaya. Alikaa Moreshethi, mji uliokuwa kusini-magharibi mwa Yerusalemu. Hali ya nyakati alizoishi nabii huyu inaonekana katika sura tano za kwanza za kitabu hiki. Alihubiri kwamba Samaria, uliokuwa mji mkuu wa utawala wa kaskazini, yaani Israeli, ungeshambuliwa na kutekwa. Aliamini pia kwamba utawala wa Yuda ungekumbwa pia na balaa hilo la kitaifa. Alitangaza pia kuharibiwa kwa hekalu, jambo ambalo wakati huo lilidhaniwa kuwa haliwezekani. Katika mahubiri yake, Mika aliwashutumu hasa wakuu wa watu: Matajiri, watawala, mahakimu, makuhani na manabii ambao waliwakosesha watu.
Baadhi ya mambo yanayoweza kutajwa hapa kwa umuhimu wake ni ahadi ya amani ulimwenguni chini ya utawala wake Mungu (4:1-4); maneno kuhusu mfalme atakayekuja – kutoka Bethlehemu – maneno ambayo yanatajwa pia katika Agano Jipya (5:4 Taz Mat 2:6 na Yoh 7:42) na maneno muhimu sana ya 6:8: Kwamba anachotaka Mwenyezi-Mungu kutoka kwako ni hiki: “Utende mambo ya haki, utende mema, na kuishi kwa unyenyekevu na Mungu wako.”

Currently Selected:

Mika UTANGULIZI: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy