Malaki 1
1
1Kauli ya Mwenyezi-Mungu iliyomjia Malaki awaambie Waisraeli.
Mwenyezi-Mungu anawapenda Waisraeli
2 # 1:2-3 Taz Rom 9:13 # 1:2-5 Taz Isa 34:5-17; 63:1-6; Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; 35:1-15; Amo 1:11-12; Oba 1-14Mwenyezi-Mungu asema: “Daima nimewapenda nyinyi”. Lakini watu wa Israeli wanauliza, “Umetupendaje?” Naye Mwenyezi-Mungu asema: “Je, Esau hakuwa ndugu yake Yakobo? Hata hivyo nilimpenda Yakobo 3nikamchukia Esau. Nimeiharibu nchi ya milima ya Esau ambayo ni urithi wake, nikawaachia mbwamwitu wa jangwani. Nao wazawa 4wa Esau, yaani Waedomu, wanasema kwamba ingawa miji yao imeharibiwa, watajenga upya magofu yake. Lakini, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema kwamba wanaweza kuijenga upya, lakini mimi nitaibomolea mbali. Watu watawaita, ‘Taifa ovu ambalo Mwenyezi-Mungu amelikasirikia milele.’ 5Nanyi mtakapoyaona hayo kwa macho yenu, mtatambua na kusema: ‘Ukuu wa Mwenyezi-Mungu wafika hata nje ya mipaka ya nchi ya Israeli.’”
Mwenyezi-Mungu awakaripia makuhani
6Mwenyezi-Mungu wa majeshi anawaambia hivi nyinyi makuhani mnaolidharau jina lake: “Mtoto humheshimu mzazi wake, na mtumishi humheshimu bwana wake. Ikiwa mimi ndiye Baba yenu, mbona mwanivunjia heshima? Ikiwa mimi ni bwana wenu, mbona hamniheshimu? Nanyi mnauliza, ‘Sisi tumekudharauje?’ 7Mwanidharau kwa kunitolea madhabahuni pangu tambiko ya chakula najisi. Lakini nyinyi mnauliza, ‘Tumekitiaje najisi?’ Mnakitia najisi kwa kuidharau madhabahu yangu. 8#Taz Kumb 15:21 Mnaponitolea tambiko ya mnyama kipofu, au kilema, au mgonjwa, je, huo si uovu? Je, mtawala atapendezwa au kukufanyia hisani ukimpa zawadi ya mnyama kama huyo?”
9Kwa hiyo sasa enyi makuhani, mwombeni Mungu ili atuhurumie. Ikiwa mnamtolea matoleo ya aina hiyo, je, kweli atakuwa radhi nanyi? 10Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema, “Laiti angepatikana mtu mmoja miongoni mwenu ambaye angefunga milango ya hekalu ili msiwashe moto usiokubalika kwenye madhabahu yangu! Sipendezwi nanyi na sitaikubali tambiko yoyote mnayonitolea. 11Watu wa mataifa kote duniani, toka mawio ya jua hadi machweo yake, wanalitukuza jina langu. Kila mahali wananifukizia ubani na kunitolea tambiko zinazokubalika; maana jina langu linatukuzwa miongoni mwao. 12Lakini nyinyi mnalibeza jina langu pale mnapoichafua madhabahu yangu, na chakula mnachotoa juu yake mnakidharau. 13Mnasema, ‘Mambo haya yametuchosha mno,’ na mnanidharau. Mnaniletea tambiko za wanyama mliowapata kwa unyang'anyi, au walio vilema au wagonjwa. Je, nipokee tambiko hizo mikononi mwenu? Mimi Mwenyezi-Mungu nauliza. 14Na alaaniwe mtu yeyote anidanganyaye, ambaye huahidi kwa kiapo kunitolea tambiko mnyama safi kutoka katika kundi lake, lakini hunitolea tambiko mnyama mwenye kilema. Tazama, mimi ni mfalme mkuu, na watu wa mataifa yote hunicha.”
Currently Selected:
Malaki 1: BHN
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Malachi 1
1
1The burden of the word of the Lord to Israel by Malachi.
Israel Beloved of God
2“I#Deut. 4:37; 7:8; 23:5; Is. 41:8, 9; (Jer. 31:3); John 15:12 have loved you,” says the Lord.
“Yet you say, ‘In what way have You loved us?’
Was not Esau Jacob’s brother?”
Says the Lord.
“Yet #Rom. 9:13Jacob I have loved;
3But Esau I have hated,
And #Jer. 49:18; Ezek. 35:9, 15laid waste his mountains and his heritage
For the jackals of the wilderness.”
4Even though Edom has said,
“We have been impoverished,
But we will return and build the desolate places,”
Thus says the Lord of hosts:
“They may build, but I will #Jer. 49:16–18throw down;
They shall be called the Territory of Wickedness,
And the people against whom the Lord will have indignation forever.
5Your eyes shall see,
And you shall say,
#Ps. 35:27; Mic. 5:4‘The Lord is magnified beyond the border of Israel.’
Polluted Offerings
6“A son #(Ex. 20:12); Prov. 30:11, 17; (Matt. 15:4–8; Eph. 6:2, 3)honors his father,
And a servant his master.
#(Is. 63:16; 64:8); Jer. 31:9; Luke 6:46If then I am the Father,
Where is My honor?
And if I am a Master,
Where is My reverence?
Says the Lord of hosts
To you priests who despise My name.
#Mal. 2:14Yet you say, ‘In what way have we despised Your name?’
7“You offer #Deut. 15:21defiled food on My altar,
But say,
‘In what way have we defiled You?’
By saying,
#Ezek. 41:22‘The table of the Lord is contemptible.’
8And #Lev. 22:22; Deut. 15:19–23when you offer the blind as a sacrifice,
Is it not evil?
And when you offer the lame and sick,
Is it not evil?
Offer it then to your governor!
Would he be pleased with you?
Would he #(Job 42:8)accept you favorably?”
Says the Lord of hosts.
9“But now entreat God’s favor,
That He may be gracious to us.
#Hos. 13:9While this is being done by your hands,
Will He accept you favorably?”
Says the Lord of hosts.
10“Who is there even among you who would shut the doors,
#1 Cor. 9:13So that you would not kindle fire on My altar in vain?
I have no pleasure in you,”
Says the Lord of hosts,
#Is. 1:11“Nor will I accept an offering from your hands.
11For #Is. 59:19from the rising of the sun, even to its going down,
My name shall be great #Is. 60:3, 5among the Gentiles;
#1 Tim. 2:8In every place #Rev. 8:3incense shall be offered to My name,
And a pure offering;
#Is. 66:18, 19For My name shall be great among the nations,”
Says the Lord of hosts.
12“But you profane it,
In that you say,
#Mal. 1:7‘The table of the Lord is defiled;
And its fruit, its food, is contemptible.’
13You also say,
‘Oh, what a #Is. 43:22weariness!’
And you sneer at it,”
Says the Lord of hosts.
“And you bring the stolen, the lame, and the sick;
Thus you bring an offering!
#Lev. 22:20Should I accept this from your hand?”
Says the Lord.
14“But cursed be #Mal. 1:8the deceiver
Who has in his flock a male,
And takes a vow,
But sacrifices to the Lord #Lev. 22:18–20what is blemished—
For #Ps. 47:2I am a great King,”
Says the Lord of hosts,
“And My name is to be feared among the nations.
The Holy Bible, New King James Version, Copyright © 1982 Thomas Nelson. All rights reserved.