YouVersion Logo
Search Icon

Waebrania 8

8
Yesu kuhani wetu mkuu
1 # Taz Zab 110:1 Basi, jambo muhimu katika hayo tunayosema ni hili: Sisi tunaye kuhani mkuu wa namna hiyo, ambaye anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mkuu mbinguni. 2Yeye hutoa huduma ya kuhani mkuu mahali patakatifu katika maskani, yaani ndani ya ile hema ya kweli iliyojengwa na Bwana, siyo na binadamu.
3Kila kuhani mkuu ameteuliwa kumtolea Mungu zawadi na tambiko, na hivyo kuhani mkuu wetu lazima naye awe na kitu cha kutolea. 4Kama yeye angekuwa wa hapa duniani, asingekuwa kamwe kuhani, kwani wako makuhani wengine wanaotoa sadaka kufuatana na sheria. 5Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Maana Mose alipokuwa karibu kuitengeneza ile maskani, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano uliooneshwa kule mlimani.” 6Lakini sasa Yesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo bora kuliko yao, kama vile agano alilothibitisha kati ya watu na Mungu ni bora zaidi, kwani lina msingi wake katika ahadi za mambo yaliyo bora zaidi.
7Maana kama lile agano la kwanza halingalikuwa na dosari, hakungalikuwa na haja ya agano la pili. 8Lakini Mungu aliwalaumu watu wake aliposema:
“Siku zinakuja, asema Bwana,
ambapo nitafanya agano jipya
na watu wa Israeli na wa Yuda.
9Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na babu zao
siku nilipowaongoza kwa mkono kutoka Misri.
Hawakuwa waaminifu kwa agano langu;
na hivyo mimi sikuwajali, asema Bwana.
10Hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana:
Nitaweka sheria zangu akilini mwao,
na kuziandika mioyoni mwao.
Mimi nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu.
11Hakuna atakayemfundisha mwananchi mwenzake,
wala atakayemwambia ndugu yake:
‘Mjue Bwana’.
Maana wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.
12Nitawasamehe makosa yao,
wala sitakumbuka tena dhambi zao.”
13Kwa kusema juu ya agano jipya, Mungu alilichakaza lile la kwanza; na chochote kinachochakaa na kuwa kikuukuu kitatoweka karibuni.

Currently Selected:

Waebrania 8: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy