Ndiyo maana hata mawe yatalalamika ukutani, na boriti za nyumba zitayaunga mkono. “Ole wako unayejenga mji kwa mauaji unayesimika jiji kwa maovu! Mwenyezi-Mungu wa majeshi husababisha juhudi za watu zipotelee motoni, na mataifa yajishughulishe bure. Utukufu wa Mwenyezi-Mungu utaenea pote duniani, kama vile maji yaeneavyo baharini. Ole wako unayewalewesha jirani zako, na kutia sumu katika divai yao ili upate kuwaona wamekaa uchi. Utajaa aibu badala ya heshima. Utakunywa wewe mwenyewe na kupepesuka! Mwenyezi-Mungu mwenyewe atakulevya, na aibu itaifunika heshima yako! Maovu uliyoitenda Lebanoni yatakuvamia wewe; uliwaua wanyama, wanyama nao watakutisha. Yote hayo yatakupata wewe, kwa mauaji na dhuluma uliyoitendea dunia, naam, uliyoifanyia miji na wakazi wake wote. “Chafaa nini kinyago alichotengeneza mtu? Sanamu ni madini yaliyoyeyushwa, ni kitu cha kueneza udanganyifu! Mtengeneza sanamu hutumaini alichotengeneza mwenyewe, kinyago ambacho hakiwezi hata kusema! Ole wake mtu aliambiaye gogo: ‘Amka!’ Au jiwe bubu ‘Inuka!’ Je, sanamu yaweza kumfundisha mtu? Tazama imepakwa dhahabu na fedha, lakini haina uhai wowote.” Lakini Mwenyezi-Mungu yumo katika hekalu lake takatifu; dunia yote na ikae kimya mbele yake.
Read Habakuki 2
Share
Compare All Versions: Habakuki 2:11-20
Save verses, read offline, watch teaching clips, and more!
YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy
Home
Bible
Plans
Videos