YouVersion Logo
Search Icon

Hekima ya Solomoni UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu hiki yaonekana kiliandikwa ili kutia moyo na kufunza jumuiya ya Wayahudi wakati wa dhiki na udhalimu wa kisiasa kikiwa na shabaha ya kuihakikishia jumuiya hiyo kwamba Mungu atawatunza wale wanaosimama imara katika imani yao.
Sura 1–5 zina mawaidha juu ya miisho tofauti ya waaminifu na ya watu waovu. Zagusia dhahiri juu ya maisha ya milele baada ya kifo (taz pia Dan 12:2-3).
Sura 6:1–9:12 zina sifa za Hekima. Hekima ni kitu cha lazima kwa wote hasa kwa wale walio na jukumu la kuyaongoza mataifa. Ili kuelezea jambo hilo mwandishi, anajifanya kuwa sawa na Solomoni ambaye mapokeo ya Wayahudi yalimtambua kuwa mwenye hekima mkuu (linganisha na 1Fal 3:4-15; 4:29-34).
Sehemu ya tatu yaani sura 9:13–19:22 yazungumzia juu ya Hekima kwa mifano inayotokana na historia ya watu wa Israeli. Mwandishi anatafakari juu ya masimulizi ya kitabu cha Mwanzo na hasa kitabu cha Kutoka. Mwandishi anaeleza upya au anafafanua masimulizi ya Biblia kwa kutumia fikira za Kigiriki. Humu tunapata habari kadhaa ambazo hazimo dhahiri mahala pengine katika Agano la Kale kama vile kuachana kwa roho na mwili (9:15) kwamba roho haifi (3:14; 8:17; 15:3 n.k.).

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy