YouVersion Logo
Search Icon

Ezekieli 2

2
Ezekieli anaitwa kuwa nabii
1Naye akaniambia, “Wewe mtu! Simama wima. Nataka kuongea nawe.” 2Alipokuwa akiongea nami, roho ya Mungu ikaniingia na kunisimamisha wima. Ndipo nikamsikia 3akiniambia, “Wewe mtu#2:3 Mtu: Kiebrania ben'adam: Jina linalotumiwa mara nyingi katika Ezekieli. Msemo huo wataka kukumbusha kwamba mtu ni kiumbe (sio Mungu) na ana hali yake hafifu na hufa kwa hiyo huhitaji nguvu ya Mungu kumwongoza. nakutuma kwa Waisraeli, taifa#2:3 taifa: Makala ya Kiebrania: Mataifa. la waasi ambao wameniasi. Wameendelea kunikosea mimi hadi leo kama walivyokuwa wazee wao. 4Watu hao ni wafidhuli na wajeuri. Nakutuma kwao, nawe utawaambia kwamba mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi na hivi. 5Wakisikia au wasiposikia, maana wao ni watu waasi, walau watatambua kwamba nabii amekuwapo miongoni mwao. 6Lakini, ewe mtu usiwaogope hao wala maneno yao. Hata kama mbigili na miiba vinakuzunguka, au unaketi juu ya nge, usiogope maneno yao wala usitishwe na nyuso zao, kwani hao ni watu waasi. 7Wewe utawaambia maneno yangu, hata kama watasikia au hawatasikia, maana wao ni watu waasi.
8“Lakini ewe mtu, sikiliza ninayokuambia, wala usiwe mwasi kama watu hao. Fumbua kinywa chako, ule ninachokupa.” 9# 2:9-10 Taz Ufu 5:1 Nilipotazama, niliona nimenyoshewa mkono, na kumbe ulikuwa na kitabu kilichoandikwa. 10Basi akakifungua mbele yangu, nacho kilikuwa kimeandikwa mbele na nyuma maneno ya maombolezo, vilio na laana.

Currently Selected:

Ezekieli 2: BHND

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy