YouVersion Logo
Search Icon

1 Mambo ya Nyakati 3

3
Wana wa mfalme Daudi
1Hawa ndio wana wa mfalme Daudi waliozaliwa wakati alipokuwa huko Hebroni:
Amnoni, mzaliwa wake wa kwanza; mama yake aliitwa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili, Mkarmeli; 2wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, bintiye Talmai mfalme wa Geshuri; wa nne alikuwa Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi; 3wa tano alikuwa Shefatia, ambaye mama yake alikuwa Abitali; na wa sita alikuwa Ithreamu, ambaye mama yake alikuwa Egla.
4Wote sita, walizaliwa Hebroni ambako Daudi alitawala kwa muda wa miaka saba na nusu. Huko Yerusalemu, alitawala kwa muda wa miaka thelathini na mitatu. 5Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: Mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni.
6Na mbali na hao alikuwa na wana wengine tisa: Ibhari, Elishua, Elifaleti, 7Noga, Nefegi, Yafia, 8Elishama, Eliada na Elifeleti. 9Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wengine waliozaliwa na masuria wake. Daudi alikuwa na binti pia, aliyeitwa Tamari.
Wazawa wa mfalme Solomoni
10Wazawa wa mfalme Solomoni: Solomoni alimzaa Rehoboamu, aliyemzaa Abiya, aliyemzaa Asa, aliyemzaa Yehoshafati, 11aliyemzaa Yehoramu, aliyemzaa Ahazia, aliyemzaa Yoashi, 12aliyemzaa Amazia, aliyemzaa Uzia, aliyemzaa Yothamu, 13aliyemzaa Ahazi, aliyemzaa Hezekia, aliyemzaa Manase, 14aliyemzaa Amoni, aliyemzaa Yosia. 15Yosia alikuwa na wana wanne: Yohanani, mzaliwa wake wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia na wa nne Shalumu. 16Yehoyakimu alikuwa na wana wawili: Yekonia na Sedekia.
17Wana wa Yekonia aliyechukuliwa mateka na Wababuloni walikuwa saba: Shealtieli, 18Malkiramu, Pedaya, Shenazari, Yekamia, Hoshama na Nedabia. 19Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Zerubabeli alikuwa na wana wawili: Meshulamu na Hanania, na binti mmoja, jina lake Shelomithi. 20Zerubabeli pia alikuwa na wana wengine watano: Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-hesedi. 21Wana wa Hanania walikuwa Pelatia na Yeshaya. Yeshaya alimzaa Refaya, aliyemzaa Arnani, aliyemzaa Obadia, aliyemzaa Shekania.#3:21 aya hii Kiebrania si dhahiri. 22Shekania alimzaa Shemaya. Wana wa Shemaya walikuwa sita: Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati. 23Nearia alikuwa na wana watatu: Eliehonai, Hizkia na Azrikamu. 24Eliehonai alikuwa na wana saba: Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani.

Currently Selected:

1 Mambo ya Nyakati 3: BHND

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy