Skip to content

Yakobo 2

2
Mpendane, lakini msipendelee!
1Ndugu zangu, msiwaze kwamba: Kumtegemea Bwana wetu mtukufu Yesu Kristo hupatana na kupendelea watu!#1 Kor. 2:8. 2Ni hivyo: mle mkutaniamo mkiingia mtu mwenye pete za dhahabu vidoleni, aliyevaa mavazi mazuri, tena mkiingia hata maskini mwenye mavazi machakavu, 3nanyi mkamtazama yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia: Wewe kaa hapa pazuri! kisha mkamwambia yule maskini: Wewe simama huko au kaa hapa chini miguuni pangu! 4je? Hivyo mioyo yenu haikujiumbua kwamba: Mkiwagawanya hivyo mmefuata mawazo mabaya? 5Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa! Mungu hakuwachagua walio maskini ulimwenguni, wawe wenye mali kwa kumtegemea, tena wautwae ufalme, aliowaagia wampendao, uwe urithi wao?#Luk. 12:21; 1 Kor. 1:26. 6Lakini ninyi mmemnyima maskini heshima. Wenye mali sio wanaowaendea ninyi kwa nguvu? Sio wanaowaburura bomani? 7Nao sio wanaolitukana lile Jina zuri, mwitwalo nalo?#1 Petr. 4:14. 8Kweli, mkilitimiza Agano la kifalme, kama lilivyoandikwa kwamba: Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe! mnafanya vizuri.#3 Mose 19:18. 9Lakini mkiwapendelea watu mnakosa, mkajulishwa na hilo agizo waziwazi kuwa wenye kulipita.#5 Mose 1:17.
10*Kwani mtu akiyashika Maonyo yote akalikosea moja tu, amekwisha kuyakosea yote.#Mat. 5:19. 11Kwani yeye aliyesema: Usizini! ndiye aliyesema: Usiue! Nawe usipozini, lakini unaua, basi, umekwisha kuwa mwenye kuyapita Maonyo.#2 Mose 20:13-14. 12Semeni, tena fanyeni hivyo, kama watu wafanyavyo watakaohukumiwa kwa Maonyo yanayotupatia kukombolewa!#Yak. 1:25. 13Kwani mtu akosaye huruma atapata naye hukumu ikosayo huruma; lakini huruma hushangilia nako kwenye hukumu.#Mat. 5:7; 18:30,34; 25:45,46.
Kumtegemea Mungu pasipo matendo ni kwa bure.
14Ndugu zangu, mtu akisema: Niko na kumtegemea Mungu, lakini matendo hanayo, inamfaliaje? Kumtegemea Mungu kunaweza kumwokoa?#Mat. 7:21. 15Kwetu kukipatikana ndugu mume au mke walio wenye uchi na wenye kukosa chakula cha siku moja tu, 16mtu wa kwenu akawaambia: Nendeni na kutengemana, mwote moto, mpate kushiba! asiwape yaipasayo miili yao, itawafaliaje?#1 Yoh. 3:17. 17Hapo mwaona: Kumtegemea Mungu kusikoendelea na matendo yakupasayo kumekwisha kuangamika kwenyewe.* 18Labda yuko atakayesema: Wewe uko na kumtegemea Mungu, nami niko na matendo; nionyesha, unavyomtegemea Mungu pasipo matendo! kisha nami nitakuonyesha, matendo yangu yanavyotimilika katika kumtegemea Mungu.#Gal. 5:6. 19Wewe unaamini, ya kuwa Mungu ni mmoja tu? Ni vizuri; pepo nao huyaamini hayo, lakini hutetemeka!#Mat. 8:29. 20Mtu mpuzi, unataka kutambua, ya kuwa kumtegemea Mungu kusikoendelea na matendo ni kwa bure? 21Baba yetu Aburahamu hakupata wongofu kwa matendo alipompeleka mwana wake Isaka, awe ng'ombe ya tambiko?#1 Mose 22:9-10,12; Ebr. 11:17. 22Unaona: Kumtegemea Mungu husaidiana na matendo yakupasayo; napo, alipofanya yampasayo, ndipo, kumtegemea Mungu kulipotimilika kwake, 23nayo yaliyoandikwa yakatimia kwamba:
Aburahamu alimtegemea Mungu,
kwa hiyo akawaziwa kuwa mwenye wongofu,
akaitwa mpenzi wake Mungu.#1 Mose 15:6; Yes. 41:8. 24Mnaona: Mtu hupata wongofu kwa matendo, siko kwa kumtegemea Mungu tu. 25Tena je? Yule mke mgoni Rahabu hakupata wongofu naye kwa matendo, alipowafikiza wale wajumbe na kuwatoa mjini kwa njia nyingine?#Yos. 2:4,15; Ebr. 11:31. 26Kwani kama mwili unavyokufa, usipopumua, vivyo hivyo nako kumtegemea Mungu kusikoendelea na matendo kunakufa.#Yak. 2:17.