Hosea 3
3
Kwa uvumilivu Mungu atawapata walio ukoo wake.
1Bwana akaniambia: Nenda tena kumpenda mwanamke mzinzi anayependwa na mwingine, kama Bwana anavyowapenda wana wa Isiraeli, nao huigeukia miungu mingine kwa kuyapenda maandazi ya zabibu.#Hos. 1:2. 2Nikamnunua, awe wangu, nikatoa fedha kumi na tano na frasila kumi na tano za mawele. 3Nikamwambia: Siku nyingi utakaa tu kwangu, usizini, wala usiwe wa mume; mimi nami nitakuwa vivyo hivyo kwako. 4Kwani wana wa Isiraeli watakaa siku nyingi pasipo mfalme wala mkuu, pasipo tambiko wala kinyago, pasipo vazi la mtambikaji wala Patakatifu.#2 Mambo 15:3. 5Kisha wana wa Isiraeli watarudi, wamtafute Bwana Mungu wao na Dawidi, mfalme wao; siku zitakazokuwa za mwisho watamwendea Bwana na wema wake kwa kutetemeka.#Yer. 30:9,21-22; Ez. 34:23-24.
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.