Skip to content

2 Watesalonike 3

3
Anawahimiza, wamwombee.
1Kisha, ndugu, mtuombee sisi kwa Mungu, Neno la Bwana liendelee na kutukuzwa vivyo hivyo kama kwenu!#Kol. 4:3. 2Tena tuombeeni, tuokolewe mikononi mwa watu walio wapuzi na wabaya! Kwani sio wote wawezao kumtegemea Bwana. 3Lakini Bwana ni mwelekevu atakayewashupaza na kuwalinda, yule Mbaya asiwajie.#1 Tes. 5:24. 4Kwa ajili yenu tunamtumaini Bwana kwamba: Tunayowaagiza, mwayashika sasa, hata siku za nyuma mtayashika.#2 Kor. 7:16; Gal. 5:10. 5Bwana aiongoze mioyo yenu, iufikie upendo wa Mungu na uvumilivu wa Kristo!
Anawaonya wasiofanya kazi.
6*Ndugu, tunawaagiza ninyi, kwa nguvu ya Jina la Bwana Yesu Kristo, mtengane na kila ndugu anayeendelea na kufuata mambo yaliyo ya ovyoovyo tu, asiufuate ufundisho, mlioupata kwetu sisi.#Mat. 18:15-17; Rom. 16:17. 7Kwani mwajua wenyewe, jinsi inavyowapasa kutuiga, kwa sababu hatukukaa kwenu kiovyoovyo tu.#1 Tes. 1:6. 8Hakuna, ambaye tulikula chakula chake bure, ila tulijisumbua na kujiumiza tukifanya kazi usiku na mchana kwa kukataa kumlemea mtu ye yote wa kwenu.#1 Kor. 4:12. 9Hatukuvifanya hivyo kwamba: Hatu wakuu, ila tulitaka kuwapa ninyi vielezo, mpate kutuiga.#Mat. 10:10; 1 Kor. 4:16. 10Kwani tulipokuwa kwenu tuliwaagiza hata neno hili: Mtu asiyetaka kufanya kazi asipate chakula!#1 Mose 3:19; 2 Mose 20:9. 11Kwani twasikia: Kwenu wako wanaoendelea na kufuata mambo yaliyo ya ovyoovyo tu, hawafanyi kazi, ila hufanya mapuzi.#1 Tim. 1:6. 12Walio hivyo tunawaagiza na kuwaonya machoni pake Bwana Yesu Kristo, watulie, wapate kufanya kazi na kula chakula chao wenyewe.#1 Tes. 4:11. 13Lakini ninyi, ndugu, msichoke kufanya yaliyo mazuri!*#Gal. 6:9. 14Lakini mtu asipoyatii maneno yetu yaliyomo humu baruani, huyo mjulisheni mkikataa kuchanganika naye, apatwe na soni!#2 Tes. 3:6; 1 Kor. 5:9,11. 15Lakini msimwazie kuwa mchukivu, ila mwonyeni kindugu! 16Lakini yeye Bwana aliye mwenye utangemano awape kutengemana po pote katika mambo yote! Bwana awe nanyi nyote!#Yoh. 14:27.
17Salamu hii naiandika kwa mkono wangu mimi Paulo; huu ndio mwandiko wangu katika barua zote. Hivi ndivyo, ninavyoandika.#1 Kor. 16:21. 18Upole wa Bwana wetu Yesu Kristo uwakalie ninyi nyote! Amin.