Zaburi 8
8
Utukufu wa Mungu na cheo cha mwanadamu
1Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa mutindo wa watu wa Gati. Zaburi ya Daudi.
2Ee Yawe, Bwana wetu,
jina lako linatukuzwa sana katika dunia yote!
Utukufu wako unaenea mpaka juu ya mbingu!
3Kutoka maneno ya watoto wadogo, hata wachanga,
unaimarisha nguvu mbele ya waadui zako
na kuwakomesha waasi na wapinzani wako.
4Nikiangalia mbingu uliyoumba kwa vidole vyako,
mwezi na nyota ulizozisimika huko,
5mutu ni nini, ee Mungu, hata umufikirie?
Mwanadamu ni nini hata umujali? #Ang. Zab 144.3; Ebr 2.6-8
6Umemufanya kuwa karibu sawa na Mungu,
umemujaza utukufu na heshima.
7Ulimupa utawala juu ya vyote ulivyoviumba;
uliweka viumbe vyote chini ya mamlaka yake: #Ang. 1 Kor 15.27; Efe 1.22; Ebr 2.8
8kondoo, ngombe,
na nyama wa pori,
9ndege, samaki,
na viumbe vyote vya bahari.
10Ee Yawe, Bwana wetu,
jina lako linatukuzwa sana katika dunia yote!
Currently Selected:
Zaburi 8: SWC02
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.