Bible App logo
Search Icon

Zaburi 70

70
Kuomba musaada
(Zab 40.13-17)
1Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi inayoelekea sadaka yake ya ukumbusho.
2Ee Mungu,
uniokoe!
Ee Yawe,
ukuje haraka unisaidie.
3Wapate haya na kufezeheka wanaotaka kuniua!
Warudi nyuma na kufezeheka wanaonitakia hasara!
4Wapumbazike kwa haya,
hao wanaofurahia kunizomea!
5Lakini wote wanaokutafuta,
wafurahi na kushangilia kwa sababu yako.
Wote wanaopenda wokovu wako,
waseme siku zote: “Mungu ni mukubwa!”
6Nami ninayekuwa masikini na mukosefu,
unifikie haraka, ee Mungu!
Wewe ndiwe musaada wangu na mukombozi wangu.
Ee Yawe, usikawie!

Currently Selected:

Zaburi 70: SWC02

Highlight

Copy

Compare

Share

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in