Zaburi 60
60
Ushindi nyuma ya kushindwa vita
1-2Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa mutindo wa wimbo “Ushuhuda wa mayungiyungi.” Mashairi ya Daudi ya kufundisha yanayoelekea wakati alipopigana na Wasuria katika Mesopotamia na Zoba naye Yoabu aliporudi nyuma na kuwaua Waedomu elfu kumi na mbili katika bonde la Chumvi.
3Ee Mungu,
umetutupilia na kutuponda,
umewaka hasira.
Tafazali uturudishie nguvu.
4Umeitetemesha inchi na kuipasua;
uzibe nyufa zake kwa maana imetikisika.
5Umewaletea watu wako mateso;
umetukunywesha divai tuyumbeyumbe.
6Uwaarifu kwa vitambulisho wale wanaokuheshimu,
wapate kuuepuka mushale.
7Uwaponyeshe hao watu unaowapenda!
Utuokoe kwa mukono wako!
Utusikilize!
8Mungu amesema kutoka pahali pake patakatifu:
“Sasa kwa shangwe nitaigawanya inchi ya Sekemu;
Bonde la Sukoti nitalipima sehemu sehemu.
9Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu;
Efuraimu ni kofia yangu ya chuma,
na Yuda ni fimbo yangu ya kifalme.
10Moabu ni kama bakuli langu la kunawia.
Nitatupia Edomu kiatu changu kwa kuirizi.
Nitapiga kelele la ushindi juu ya Filistia.”
11Ni nani atakayenipeleka kwenye muji unaozungukwa na kuta?
Ni nani atakayeniongoza mpaka Edomu?
12Si wewe Mungu ambaye umetutupilia?
Lakini hauendi tena na jeshi letu.
13Utusaidie kwa kuwashinda waadui zetu,
maana musaada wa mwanadamu haufai kitu.
14Mungu akikuwa upande wetu, tutashinda.
Yeye atawaponda waadui zetu.
Currently Selected:
Zaburi 60: SWC02
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.