YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 6

6
Maombi wakati wa taabu
1Kutoka Mukubwa wa waimbaji: kwa vyombo vyenye nyuzi nane. Zaburi ya Daudi.
2Ee Yawe,
usiniazibu kwa hasira yako,
usiniadibishe kwa kasirani yako. #Ang. Zab 38.2
3Unihurumie, ee Yawe, nimeishiwa nguvu;
uniponyeshe, ee Yawe, ninatetemeka mpaka katika mifupa.
4Ninahangaika sana ndani ya roho yangu.
Ee Yawe, utakawia mpaka wakati gani?
5Unigeukie, ee Yawe, uniokoe;
uniponyeshe kwa sababu ya wema wako.
6Huko kwa wafu hakuna anayekukumbuka;
katika kuzimu ni nani anayeweza kukusifu?
7Ninatabanika kwa kulia kwa uchungu;
usiku ninalowanisha kitanda changu kwa machozi;
kwa kulia kwangu ninalowanisha matandiko yangu.
8Macho yangu yamechoka kwa huzuni;
yamefifia kwa kutaabishwa na waadui.
9Muondoke karibu nami, enyi wote watenda maovu!
Maana Yawe amesikia kilio changu. #Ang. Mat 7.23; Lk 13.27
10Yawe amesikia ombi langu;
Yawe amekubali maombi yangu.
11Waadui zangu wote watafezeheka na kufazaika;
watarudi nyuma na kufezeheka kwa rafla.

Currently Selected:

Zaburi 6: SWC02

Highlight

Copy

Compare

Share

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in