Bible App logo
Search Icon

Zaburi 128

128
Baraka ya wenye kumutii Mungu
1Wimbo wa safari za kidini.
Heri wote wanaomwabudu Yawe,
wanaoishi kufuatana na amri zake.
2Utapata matunda ya jasho lako,
utafurahi na kupata uheri.
3Muke wako atakuwa kama muzabibu wenye matunda mengi;
watoto wako kama vichipukizi vya muzeituni kuzunguka meza yako.
4Kweli, hivi ndivyo atakavyobarikiwa
mutu anayemwabudu Yawe.
5Yawe akubariki kutokea Sayuni!
Uone uheri wa Yerusalema,
siku zote za maisha yako.
6Uishi na hata uwaone wajukuu wako!
Amani ikuwe na Israeli!

Currently Selected:

Zaburi 128: SWC02

Highlight

Copy

Compare

Share

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in