Bible App logo
Search Icon

Zaburi 127

127
Bila Mungu kazi ya mwanadamu haifai kitu
1Wimbo wa safari za kidini: wa Solomono.
Yawe asipoijenga nyumba,
wanaoijenga wanajisumbua bure.
Yawe asipoulinda muji,
wanaoulinda wanakesha bure.
2Munajisumbua bure kuamuka asubui mapema
na kuchelewa kwenda kupumzika magaribi,
mujipatie chakula kwa jasho lenu.
Mungu anatimiza mahitaji ya wapendwa wake hata wanapolala.
3Watoto ni urizi kutoka kwa Yawe;
uzao ni zawadi yake kwetu sisi.
4Watoto wanaokuwa na nguvu,
ni kama mishale katika mikono ya askari.
5Heri mutu anayekuwa na mishale hiyo kwa wingi.
Hatashindwa atakaposamba na waadui zake kwenye tribinali.

Currently Selected:

Zaburi 127: SWC02

Highlight

Copy

Compare

Share

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in