YouVersion Logo
Search Icon

Matayo 1

1
Kizazi cha Yesu
(Lk 3.23-38)
1-16Haya ni majina ya babu za Yesu Kristo, wa uzao wa Daudi, wa uzao wa Abrahamu.
Abrahamu alizaa Isaka,
Isaka alizaa Yakobo,
Yakobo alizaa Yuda na wandugu zake,
Yuda alizaa Peresi na Zera kutoka muke wake Tamari,
Peresi alizaa Hesironi,
Hesironi alizaa Ramu,
Ramu alizaa Aminadabu,
Aminadabu alizaa Nasoni,
Nasoni alizaa Salmoni,
Salmoni alizaa Boazi kutoka muke wake Rahaba,
Boazi alizaa Obedi kutoka muke wake Ruta,
Obedi alizaa Yese,
Yese alizaa mufalme Daudi,
Daudi alizaa Solomono (mama yake ndiye yule aliyekuwa muke wa marehemu Uria),
Solomono alizaa Rehoboamu,
Rehoboamu alizaa Abiya,
Abiya alizaa Asa#1.1-16 Asa: Katika maandiko mengine ya asili kuna jina “Asafu” pahali pa “Asa”.,
Asa alizaa Yosafati,
Yosafati alizaa Yoramu,
Yoramu alizaa Uzia,
Uzia alizaa Yotamu,
Yotamu alizaa Ahazi,
Ahazi alizaa Hezekia,
Hezekia alizaa Manase,
Manase alizaa Amoni#1.1-16 Amoni: Katika maandiko mengine ya asili kuna jina “Amozi” pahali pa “Amoni”.,
Amoni alizaa Yosia,
Yosia alizaa Yekonia na wandugu zake, wakati Waisraeli walipohamishwa kwenda Babeli.
Nyuma ya kuhamishwa kwa Waisraeli kwenda Babeli,
Yekonia alizaa Saltieli,
Saltieli alizaa Zerubabeli,
Zerubabeli alizaa Abihudi,
Abihudi alizaa Eliakimu,
Eliakimu alizaa Azoro,
Azoro alizaa Zadoki,
Zadoki alizaa Akimu,
Akimu alizaa Elihudi,
Elihudi alizaa Eleazari,
Eleazari alizaa Matani,
Matani alizaa Yakobo,
Yakobo alizaa Yosefu, yule alikuwa mume wa Maria, mama ya Yesu, anayeitwa Kristo.
17Hivi hesabu ya vizazi vyote tangia Abrahamu mpaka Daudi ni vizazi kumi na vine, na tangia Daudi mpaka Waisraeli walipohamishwa kwenda Babeli ni vizazi kumi na vine, na tangia Waisraeli walipohamishwa kwenda Babeli mpaka kuzaliwa kwa Kristo ni vizazi kumi na vine.
Kuzaliwa kwa Yesu Kristo
(Lk 2.1-7)
18Hii ndiyo habari ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Maria, mama yake, alikuwa muchumba wa Yosefu. Lakini mbele hawajakaa pamoja, akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mutakatifu. 19Yosefu, muchumba wake, alikuwa mutu wa haki, naye hakutaka kumupatisha haya mbele ya watu, akakusudia kuachana naye kwa siri. 20Naye alipokuwa angali akifikiri juu ya maneno hayo, malaika wa Bwana akamutokea katika ndoto na kumwambia hivi: “Wewe Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumwoa muchumba wako Maria, kwa maana mimba yake imetokana na uwezo wa Roho Mutakatifu. 21Yeye atazaa mutoto mwanaume, nawe utamwita jina lake Yesu#1.21 Yesu: Maana ya jina “Yesu” ni “Bwana anayeokoa”., kwa maana ndiye atakayewaokoa watu wake toka katika zambi zao.”
22Mambo hayo yote yalitukia kusudi yatimie maneno Bwana aliyosema kwa njia ya nabii:
23“Angalia bikira atapata mimba, atazaa mutoto mwanaume,
naye ataitwa Emanueli,”
(maana yake “Mungu yuko pamoja nasi”).
24Na wakati Yosefu alipoamuka, akafanya sawa vile malaika wa Bwana alivyomwagiza. Akamwoa Maria. 25Lakini hakulala naye mpaka alipozaa yule mutoto mwanaume. Yosefu akamwita jina lake Yesu.

Currently Selected:

Matayo 1: SWC02

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy