Yona 2
2
1Kisha, Yawe akaamuru samaki mukubwa amumeze Yona, naye akabaki ndani ya tumbo la samaki huyo kwa muda wa siku tatu, usiku na muchana.
Maombi ya Yona
2Basi, Yona akiwa ndani ya tumbo la samaki yule, akamwomba Yawe Mungu wake, 3akisema:
Kwa sababu ya taabu yangu,
nilikuomba, ee Yawe,
nawe ukanisikiliza;
toka chini kuzimu, nilikulilia,
nawe ukasikiliza kilio changu.
4Ulinitupa katika kilindi, katikati ya bahari,
maji mengi yakanizunguka,
mawimbi na maji mengi vikapita juu yangu.
5Nilizani kwamba nimetupwa mbali nawe;
nisiweze kuliona tena hekalu lako takatifu.
6Maji yalinizunguka na kunisonga;
kilindi kilinifikia kila upande,
majani ya bahari yakanifunika kichwa.
7Niliteremuka mpaka kwenye misingi ya milima,
katika inchi ambayo milango yake imefungwa milele.
Lakini wewe, ee Yawe, Mungu wangu,
umenipandisha nikiwa muzima kutoka mule ndani ya shimo.
8Roho yangu ilipoanza kunitoka,
nilikukumbuka, ee Yawe,
maombi yangu yakakufikia
katika hekalu lako takatifu.
9Watu wanaoabudu sanamu za miungu ya bure,
wanautupilia mbali uaminifu wao kwako.
10Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,
nitakutolea sadaka,
na kutimiza viapo vyangu.
Yawe, ndiye anayeokoa.
11Basi, Yawe akamwamuru yule samaki, naye akamutapika Yona kwenye inchi kavu.
Currently Selected:
Yona 2: SWC02
Highlight
Share
Compare
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.