Yeremia 45
45
Ahadi ya Mungu kwa Baruku
1Haya ndiyo maneno nabii Yeremia aliyosema katika mwaka wa ine wa utawala wa Yoyakimu mwana wa Yosia, mufalme wa Yuda na Baruku mwana wa Neria akayaandika katika kitabu:
2Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi juu yako wewe Baruku: 3Wewe ulisema: Ole wangu! Yawe ameongezea uchungu juu ya maumivu yangu. Nimechoka na kulalamika, wala siwezi kupumzika. 4Lakini Yawe ameniambia nikuambie:
Yawe anasema hivi: Yale niliyojenga ninayabomoa, na yale niliyopanda ninayaongoa; nitafanya hivyo katika inchi yote. 5Wewe unajitakia wewe mwenyewe mambo makubwamakubwa? Usiyatafute! Achana nayo, maana ninaleta maangamizi juu ya wanadamu wote. Pato lako ni hili: nitayaokoa maisha yako kila nafasi utakapokwenda.
–Ni ujumbe wa Yawe.
Currently Selected:
Yeremia 45: SWC02
Highlight
Share
Compare
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.