YouVersion Logo
Search Icon

Ezekieli 1

1
Kiti cha kifalme cha Mungu
1Kwa siku ya tano ya mwezi wa ine, mwaka wa makumi tatu,#1.1 Mwaka wa makumi tatu: Haijulikani ni mwaka wa nini. Labda ni umri wa Ezekieli au ni muda uliopitika tangu kutendeka kwa jambo kubwa fulani katika Israeli. wakati nilipokuwa katikati ya wale watu waliopelekwa katika uhamisho, karibu na muto Kebari, mbingu zikafunguka, nikapata maono toka kwa Mungu. #Ang. Ufu 19.11
2Katika siku ya tano ya mwezi (ulikuwa mwaka wa tano tangu mufalme Yoyakinu alipopelekwa katika uhamisho katika Babeli), #Ang. 2 Fal 24.10-16; 2 Sik 36.9-10 3neno la Yawe lilimufikia kuhani Ezekieli mwana wa Buzi, alipokuwa Babeli karibu na muto Kebari. Yawe alinijaza uwezo wake.
4Nilipoangalia niliona upepo wa zoruba unavuma kutokea upande wa kaskazini: kulikuwa wingu kubwa lililozungukwa na mwangaza, na moto ulitokea humo mufululizo na katikati ya huo moto kulikuwa kitu kinachometameta kama shaba. 5Kutoka humo nilitambua viumbe vine, ambavyo vilionekana hivi: Vilikuwa na umbo la mwanadamu. #Ang. Ufu 4.6 6Kila kimoja kilikuwa na nyuso ine na mabawa mane. 7Miguu yao ilikuwa yenye kunyooka; upande wa chini wa miguu yao ulikuwa kama kwato za miguu ya mwana-ngombe, nazo zilimetameta kama shaba safi. 8Chini ya mabawa yao, kulikuwa mikono inayokuwa sawa ya mutu. Mikono hiyo ilikuwa inaelekea kwenye pande zote ine pamoja na nyuso zao na mabawa yao. 9Incha za mabawa yao ziligusana kila bawa na bawa lingine. Vilipotembea, vilikwenda mbele moja kwa moja pasipo kugeuka. 10Juu ya nyuso zao: kila kimoja kilikuwa na uso wa mutu upande wa mbele, uso wa simba upande wa kuume, uso wa ngombe upande wa kushoto, na uso wa tai upande wa nyuma. #Ang. Eze 10.14; Ufu 4.7 11Mabawa mawili ya kila kimoja yalikuwa yamekunjuliwa juu na kugusana; na kwa mabawa yale mengine mawili, vilifunika miili yao. 12Popote roho alipotaka kwenda, ndiko vilikwenda;#1.12 Popote vilikwenda: au: Vilikwenda pahali vilipotaka kwenda. kila kimoja kilikwenda mbele moja kwa moja pasipo kugeuka. 13Katikati ya vile viumbe kulikuwa kitu kilichoonekana kama mienge ya moto iliyoangaza huku na huku kati ya hivyo viumbe. Moto huo ulikuwa ukiwaka sana na umeme ulitokea humo. 14Viumbe vile vilikwenda na kurudia mbio kama vile umeme unavyoonekana.
15Nilipokuwa nikiangalia viumbe vile, nikaona chini karibu na kila kiumbe kulikuwa gurudumu. #Ang. Eze 10.9-13 16Magurudumu hayo yalionekana kuwa ya namna moja, yanametameta kama jiwe la zabarajadi na umbo lao lilikuwa kama gurudumu ndani ya gurudumu lingine. 17Yalipotembea yalikwenda kwa pande zote ine pasipo kugeuka yanapokwenda. 18Miviringo ya hayo magurudumu ilikuwa mirefu na ya kuogopesha nayo ilikuwa inajaa macho pande zote. #Ang. Ufu 4.8 19Vile viumbe vilipokwenda, magurudumu nayo yalikwenda kandokando yao; na viumbe vile viliponyanyuka juu kutoka kwenye udongo, magurudumu hayo yaliinuka. 20Popote roho alipokwenda vilikwenda, nayo magurudumu yaliinuka pamoja navyo; maana roho ya hivyo viumbe ilikuwa katika magurudumu hayo. 21Viumbe hivyo vilipokwenda, magurudumu nayo yalikwenda; viliposimama, nayo yalisimama; vilipoinuka juu kutoka kwenye udongo, magurudumu nayo yaliinuka pamoja navyo. Maana roho wa vile viumbe vya ajabu ilikuwa katika magurudumu hayo.
22Juu ya vichwa vya vile viumbe kulikuwa kitu kinachofanana na anga, kinangaa kama kioo. #Ang. Ufu 4.6 23Viumbe vile vilisimama chini ya kitu hicho; mabawa mawili ya vile viumbe yalikuwa yamekunjuliwa, moja likielekea lingine, na kwa mabawa mengine mawili vilifunika miili yao. 24Vilipokuwa vinakwenda, nilisikia sauti ya mabawa yao; sauti ya muvumo huo ilikuwa kama ile ya maji mengi, kama sauti ya ngurumo kutoka kwa Mungu wa majeshi, na kama kelele ya jeshi. Viliposimama, vilikunja mabawa yao. 25Nilisikia sauti kutoka juu ya kitu kile kinachokuwa kama anga kilichokuwa juu ya vichwa vyao. 26Juu ya kitu hicho niliona kitu kimoja kinachofanana na kiti cha kifalme chenye rangi la jiwe la yakuti. Juu yake kulikuwa kunaikaa kitu kinachofanana na mutu. #Ang. Eze 10.1; Ufu 4.2-3 27Sehemu ya juu ya mwili wake ilingaa kama shaba, nao ulikuwa sawa unazungukwa na moto pande zote. Tokea sehemu ya chini ya mwili wake, niliona kitu kama moto. Mwangaza ulimuzunguka. #Ang. Eze 8.2 28Ulionekana kama upindi wa mvua wakati wa mvua. Ulionekana kufanana na utukufu wa Yawe. Nilipouona, nilianguka uso mpaka chini, nikasikia sauti ya mutu mwenye kusema.

Currently Selected:

Ezekieli 1: SWC02

Highlight

Share

Compare

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in