YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 121

121
Hakikisho la ulinzi wa Mungu
Wimbo wa Upandaji mlima.
1Nayainua macho yangu niitazame milima,
Msaada wangu utatoka wapi?
2Msaada wangu hutoka kwa BWANA,
Aliyezifanya mbingu na nchi.
3 # 1 Sam 2:9; Isa 27:3 Hatauacha mguu wako usogezwe;
Akulindaye hatasinzia;
4Naam, hatasinzia wala hatalala,
Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5BWANA ndiye mlinzi wako;
BWANA ni uvuli katika mkono wako wa kulia.
6 # Isa 49:10 Jua halitakupiga mchana,
Wala mwezi wakati wa usiku.
7 # Ayu 5:19; Zab 91:9,10; Mit 12:21 BWANA atakulinda na mabaya yote,
Atakulinda nafsi yako.
8 # Kum 28:6; Mit 2:8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo,
Tangu sasa na hata milele.

Currently Selected:

Zaburi 121: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy