YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 116:1-11

Zaburi 116:1-11 SRUV

Haleluya. Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Nilipata dhiki na mateso; Nikaliitia jina la BWANA. Ee BWANA, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. BWANA ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. BWANA huwalinda wasio na hila; Nilidhilika, akaniokoa. Ee nafsi yangu, urudi pumzikoni mwako, Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu. Maana umeniponya nafsi yangu na mauti, Macho yangu na machozi, Na miguu yangu na kuanguka. Nitaenenda mbele za BWANA Katika nchi za walio hai. Nilidumisha imani yangu, hata niliposema, Mimi nateseka sana. Nikiwa katika hangaiko langu nikasema, Wanadamu wote ni waongo.

Free Reading Plans and Devotionals related to Zaburi 116:1-11