YouVersion Logo
Search Icon

Mathayo 4

4
Majaribu ya Yesu
1 # Mk 1:12,13; Lk 4:1-13 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.#Ebr 2:18; 4:15 2#Kut 34:28; 1 Fal 19:8 Akafunga siku arubaini mchana na usiku, mwishowe akaona njaa. 3#Mwa 3:1-7 Mjaribu akamjia akamwambia, Ikiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate. 4#Kum 8:3 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. 5#Mt 27:53 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, 6#Zab 91:11-12 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa,
Atakuagizia malaika zake;
Na mikononi mwao watakuchukua;
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7 # Kum 6:16 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. 8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka katika mlima mrefu mno, akamwonesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, 9akamwambia, Haya yote nitakupa, ukiinama na kunisujudia. 10#Kum 6:13 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake. 11#Yn 1:51; Ebr 1:6,14 Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.
Yesu aanza huduma yake katika Galilaya
12 # Mk 1:14,15; Lk 4:14,15 Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya;#Mt 14:3; Mk 6:17; Lk 3:19-20 13#Yn 2:12 akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali; 14#Isa 9:1-2 ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
15 # Isa 9:1-2 Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,
Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani,
Galilaya ya mataifa,
16Watu wale waliokaa katika giza
Wameona mwanga mkuu,
Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti
Mwanga umewazukia.
17 # Mt 3:2 Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Yesu awaita wanafunzi wa kwanza
18 # Mk 1:16-20; Lk 5:1-11 Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.#Yn 1:40 19#Mt 13:47; Eze 47:10 Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. 20#Mt 19:27 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. 21Alipoendelea, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwa katika mashua pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita. 22Mara wakaiacha mashua na baba yao, wakamfuata.
Yesu awahudumia makundi ya watu
23 # Mt 9:35; Mk 1:39; Lk 4:15,44; Mdo 10:38 Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu. 24#Mk 6:55 Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya. 25#Mk 3:7,8; Lk 6:17-19 Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Yudea, na ng'ambo ya Yordani.

Currently Selected:

Mathayo 4: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy