YouVersion Logo
Search Icon

Mathayo 12

12
Kuvunja masuke siku ya sabato
1 # Mk 2:23-28; Lk 6:1-5 Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala.#Kum 5:14; 23:25 2#Kut 20:10 Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo ambalo si halali kulifanya siku ya sabato. 3#1 Sam 21:1-7 Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe? 4#Law 24:9 Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao? 5#Hes 28:9-10 Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato pasipo kupata hatia? 6Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu. 7#Mt 9:13; Hos 6:6 Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia. 8Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
Mwenye mkono uliopooza
9 # Mk 3:1-6; Lk 6:6-11 Akaondoka huko, akaingia katika sinagogi lao. 10#Lk 14:3 Na tazama, yumo mtu mwenye mkono umepooza; wakamwuliza, wakisema, Ni halali kuponya watu siku ya sabato? Ili wapate kumshitaki. 11#Lk 14:5 Akawaambia, Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, na yule kondoo ametumbukia shimoni siku ya sabato, asiyemshika akamwopoa? 12#Lk 14:5 Je! Mtu ni bora kuliko kondoo mara ngapi? Basi ni halali kutenda mema siku ya sabato. 13Kisha akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, ukawa mzima kama ule mwingine. 14#Yn 5:16 Lakini wale Mafarisayo wakatoka wakafanya shauri juu yake jinsi ya kumwangamiza.
Mtumishi mteule wa Mungu
15 # Mk 3:7-12 Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote, 16#Mt 8:4 akawakataza wasimdhihirishe; 17#Isa 42:1-4; 41:9 ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
18 # Isa 42:1-3 Tazama, mtumishi wangu niliyemteua;
Mpendwa wangu, moyo wangu uliyependezwa naye;
Nitatia roho yangu juu yake,
Naye atawatangazia Mataifa hukumu.#Mt 3:17
19Hatateta wala hatapaza sauti yake;
Wala mtu hatasikia sauti yake njiani.
20Mwanzi uliopondeka hatauvunja,
Wala utambi utokao moshi hatauzima,
Hadi ailetapo hukumu ikashinda.
21Na jina lake Mataifa watalitumainia.
Yesu na Beelzebuli
22 # Mk 3:22-30; Lk 11:14-26,29-32 Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona. 23Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi? 24#Mt 9:34; 10:25 Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo. 25Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yoyote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama. 26Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje? 27Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu. 28#1 Yoh 3:8 Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajia. 29#Isa 49:24; 1 Yoh 4:4 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake. 30#Mk 9:40; Yn 11:52 Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya. 31#Ebr 6:4,6; 10:26; 1 Yoh 5:16 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. 32#Lk 12:10; 1 Tim 1:13 Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.
Mti na matunda yake
33 # Mt 7:17,20; Lk 6:44 Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana. 34#Mt 3:7; 23:33; 15:18; Lk 3:7; 6:45; Yn 8:43; 12:39; Rum 8:7 Enyi wazawa wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. 35#Lk 6:45 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya. 36Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. 37Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.
Ishara ya Yona
38 # Mt 16:1; Mk 8:11; Lk 11:16; 1 Kor 1:22 Hapo baadhi ya Waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. 39#Mt 16:4; Mk 8:12 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona. 40#Yn 1:17; 2:1,2 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. 41#Yon 3:5 Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao Waninawi watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. 42#1 Fal 10:1-10; 2 Nya 9:1-12 Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.
Kurudi kwa pepo mchafu
43Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. 44Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. 45#2 Pet 2:20 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Jamaa halisi wa Yesu
46 # Mk 3:31-35; Lk 8:19-21 Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye.#Mt 13:55 47Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe. 48#Lk 2:49 Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? 49Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! 50#Rum 8:29; Yn 15:14 Kwa maana yeyote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye kaka yangu, na dada yangu na mama yangu.

Currently Selected:

Mathayo 12: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy