YouVersion Logo
Search Icon

Yohana 12

12
Mariamu ampaka Yesu mafuta
1 # Mt 26:6-13; Mk 14:3-9 Basi, siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alifika Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu. #Yn 11:1,43 2#Lk 10:40 Basi wakamwandalia karamu huko; naye Martha akatumikia; na Lazaro alikuwa mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye. 3#Lk 7:38 Basi Mariamu akatwaa ratili ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu. 4Basi Yuda Iskarioti, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema, 5Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini? 6#Lk 8:3 Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwizi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo. 7Basi Yesu alisema, Mwache aiweke kwa siku ya maziko yangu. 8#Kum 15:11 Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamko nami sikuzote.
Njama za kumwua Lazaro
9Basi watu wengi katika Wayahudi walipata kujua ya kuwa yeye yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, ila wamwone na Lazaro, ambaye Yesu alimfufua katika wafu. 10Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye; 11maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walijitenga, wakamwamini Yesu.
Yesu aingia Yerusalemu kwa ushindi
12 # Mt 21:1-11; Mk 11:1-10; Lk 19:29-40 Nayo kesho yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu; 13#Zab 118:25,26 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli! 14#Zek 9:9 Naye Yesu alikuwa amepata mwanapunda, akampanda, kama vile iliyoandikwa, 15Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda. 16#Yn 7:39 Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo. 17Basi wakamshuhudia wale mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua. 18Na kwa sababu hiyo mkutano walikwenda kumlaki, kwa kuwa wamesikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo. 19#Yn 11:48 Basi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno lolote; tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.
Baadhi ya Wagiriki wataka kumwona Yesu
20 # Yn 7:35; 11:55 Palikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu. 21#Yn 1:44; Lk 19:3; 23:8 Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu. 22Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu. 23Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu. 24#Rum 14:9; 1 Kor 15:36 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi. 25#Mt 10:39; Lk 14:26; 17:33 Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. 26#Yn 14:3; 17:24 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Yesu anena kuhusu kifo chake
27 # Zab 6:3; 42:5; Mt 26:38 Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii. 28#Yn 1:51; 5:37; Mt 3:17; 17:5 Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena. 29#Lk 22:43 Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye. 30#Yn 11:42 Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu. 31#Yn 14:30; 16:11; Lk 10:18 Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. 32#Yn 8:28 Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu. 33Aliyanena hayo akionesha ni mauti gani atakayokufa. 34#Zab 110:4; Isa 9:7; Dan 7:14 Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani? 35#Yn 8:12; 9:5; 11:10 Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Nendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako. 36#Efe 5:8; Mt 23:39 Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru.
Kutoamini kwa watu
Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha wasimwone.
37Lakini ingawa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini; 38#Isa 53:1; Rum 10:16 ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema,
Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu;
Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?
39 # Isa 6:9,10; Mt 13:14,15 Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya alisema tena,
40Amewapofusha macho,
Ameifanya mizito mioyo yao;
Wasije wakaona kwa macho yao,
Wakafahamu kwa mioyo yao,
Wakaongoka, nikawaponya.
41 # Isa 6:1 Maneno hayo aliyasema Isaya, kwa kuwa aliuona utukufu wake, akataja habari zake. 42#Yn 7:48; 9:22 Lakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi. 43#Yn 5:44 Kwa maana walipenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu.
44 # Mt 10:40 Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenituma. 45#Yn 14:9 Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenituma. 46#Yn 8:12; 12:35 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani. 47#Yn 3:17; 8:15; Lk 9:56 Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. 48#Ebr 4:12; Ufu 19:15 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. 49Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenituma, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. 50#Yn 8:26,28 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.

Currently Selected:

Yohana 12: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy