YouVersion Logo
Search Icon

Waefeso 5

5
1 # Mt 5:48; Kol 3:12 Hivyo mwigeni Mungu, kama watoto wanaopendwa; 2#Kut 29:18; Zab 40:6; Gal 2:20; Ebr 10:10; Kol 3:13; Eze 20:41 mkaende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.
Zikataeni njia za kipagani
3 # Efe 4:19; Kol 3:5 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; 4#Efe 4:29; Kol 3:8 wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali kuwepo kushukuru. 5#1 Kor 6:9,10; Kol 3:5; Mdo 8:21 Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, (ndiye mwabudu sanamu), aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. 6#Rum 1:18; Kol 2:4,8 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi. 7Basi msishirikiane nao. 8#Efe 2:11,13; Lk 16:8; 1 Pet 2:9; Yn 12:36 Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; nendeni kama watoto wa nuru, 9kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; 10#Rum 12:2 mkihakiki ni nini impendezayo Bwana. 11#Yn 16:8 Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee; 12#Rum 1:24 kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena. 13#Yn 3:20,21 Lakini chochote kinachoangazwa na nuru hudhihirishwa, maana chochote kile kilichoadhihirika ni nuru. 14#Isa 26:19; 60:1; Rum 13:11; 6:13 Hivyo husema,
Amka, wewe usinziaye,
Ufufuke katika wafu,
Na Kristo atakuangaza.
15 # Mt 10:16; Kol 4:5 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16#Kol 4:5 mkiukomboa wakati kwa maana nyakati hizi ni za uovu. 17#Rum 12:2 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana. 18#Mit 23:31; Lk 21:34 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; 19#Kol 3:16-17; Zab 33:2,3 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; 20#Kol 3:17 na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
Nyumba ya Kikristo
21 # 1 Pet 5:5 Hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.
22 # Kol 3:18; 1 Pet 3:1; Mwa 3:16 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 23#1 Kor 11:3; Kol 1:18 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. 24Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
25 # Kol 3:19; 1 Pet 3:7 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26#Tit 3:5 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27#Zab 45:13; 2 Kor 11:2 apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na dosari wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. 28Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea kanisa. 30#Efe 1:23; 1 Kor 6:15; Mwa 2:23 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. 31#Mwa 2:24 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. 32#Ufu 19:7 Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na kanisa. 33Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.

Currently Selected:

Waefeso 5: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in