YouVersion Logo
Search Icon

Luka 24

24
Kufufuka kwa Yesu
1 # Mt 28:1-8; Mk 16:1-8; Yn 20:1-13 Siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari. 2Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, 3Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu. 4Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumetameta; 5nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hadi nchini, hao waliwaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? 6#Mt 16:21; 17:22-23; 20:18-19; Mk 8:31; 9:31; 10:33-34; Lk 9:22; 18:31-33 Hayupo hapa, amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa bado yuko Galilaya, 7akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulubiwa, na kufufuka siku ya tatu. 8Wakayakumbuka maneno yake. 9Wakaondoka kaburini, wakarudi; wakawaarifu wale kumi na mmoja na wengine wote habari za mambo hayo yote. 10#Lk 8:2,3 Nao ni Mariamu Magdalene, na Yoana, na Mariamu mamaye Yakobo, na wale wanawake wengine waliokuwa pamoja nao; 11hao waliwaambia mitume habari ya mambo hayo. 12Maneno yao yakaonekana kuwa kama upuzi kwao, wala hawakuwasadiki. Lakini Petro aliondoka akaenda mbio hadi kaburini, akainama akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vya sanda tu; akaenda zake akiyastaajabia yaliyotukia.
Matembezi ya kwenda Emau
13 # Mk 16:12,13 Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda katika kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. 14Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. 15#Mt 18:20 Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. 16Macho yao yakafumbwa wasimtambue. 17Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. 18Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? 19#Mt 21:11 Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote; 20tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulubisha. 21#Lk 1:68; 2:38; 19:11; Mdo 1:6 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo; 22#Lk 24:1-11 tena, wanawake kadhaa wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, 23wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. 24#Lk 24:12; Yn 20:3-10 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona. 25Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! 26Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? 27#Kum 18:15; Zab 22:1-21; Isa 53:1-12 Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe. 28Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele. 29Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao. 30#Lk 22:19 Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. 31Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. 32Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia Maandiko? 33Wakaondoka saa ile ile, wakarejea Yerusalemu, wakawakuta wale kumi na mmoja wamekutanika, wao na wale waliokuwa pamoja nao, 34#1 Kor 15:4,5 wakisema, Bwana amefufuka kweli kweli, naye amemtokea Simoni. 35Nao waliwapa habari ya mambo yale ya njiani, na jinsi alivyotambulikana nao katika kuumega mkate.
Yesu awatokea wanafunzi wake
36 # Mk 16:14-18; Yn 20:19-23; 1 Kor 15:5 Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu. 37#Mt 14:26 Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho. 38Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu? 39Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo. 40Na baada ya kusema hayo aliwaonesha mikono yake na miguu yake. 41Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula chochote hapa? 42#Yn 21:5,10 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. 43Akakitwaa, akala mbele yao.
44 # Lk 9:22,45; 18:31-33 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa ningali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika vitabu vya Manabii na Zaburi. 45Ndipo akawafunua akili zao wapate kuelewa maandiko. 46#1 Tim 3:16 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; 47na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. 48Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. 49#Mdo 1:4; Yn 15:26; 16:7 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hadi mvikwe uwezo utokao juu.
Kupaa kwa Yesu
50 # Mdo 1:9-11 Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki. 51Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. 52#Yn 16:22; 14:28 Wakamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kuu. 53Nao daima walikuwa ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.

Currently Selected:

Luka 24: SRUVDC

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy