YouVersion Logo
Search Icon

1 Wathesalonike 5

5
1 # Mt 24:36 Lakini, ndugu, kuhusu nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. 2#Mt 24:42-44; Ufu 3:3; 16:15; Lk 12:39; 2 Pet 3:10 Maana ninyi wenyewe mnajua hakika ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwizi ajavyo usiku. 3#Yer 6:14; Yn 16:21,22; Mt 24:39; Lk 21:34,35 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. 4Bali ninyi, ndugu, hamko gizani, hata siku ile iwapate kama mwizi. 5#Rum 13:12; Efe 5:9 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza. 6Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi. 7Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku. 8#Isa 59:17; Efe 6:13-17 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. 9#1 The 1:10; 2 The 2:14 Kwa kuwa Mungu hakutuweka ili tupate hasira yake, bali ili tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo; 10#1 The 4:14; Rum 14:8,9 ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tunakesha au tunalala. 11#Yud 1:20 Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, hakika kama mnavyofanya.
Mausia ya mwisho, salamu na baraka
12 # 1 Kor 16:18; 1 Tim 5:17 Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; 13mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi.
14 # 2 The 3:6,11,15 Ndugu, tunawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote. 15#Mit 20:22; Rum 12:17; 1 Pet 3:9 Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
16 # Flp 4:4 Furahini siku zote; 17#Lk 18:1; Rum 12:12; Kol 4:2 ombeni bila kukoma; 18#Efe 5:20 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. 19#1 Kor 14:1,29,30,39 Msimzimishe Roho; 20msitweze unabii; 21#1 Yoh 4:1 jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; 22#Ayu 1:1,8; 2:3 jitengeni na ubaya wa kila namna.
23 # 2 The 3:16 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. 24#1 Kor 1:9; 2 The 3:3 Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.
25 # 2 The 3:1 Ndugu, tuombeeni. 26#1 Kor 16:20 Wasalimieni ndugu wote kwa busu takatifu. 27Nawaapisha kwa Bwana, ndugu wote wasomewe waraka huu. 28Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.

Currently Selected:

1 Wathesalonike 5: SRUVDC

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy