YouVersion Logo
Search Icon

Sef 3

3
Uovu wa Yerusalemu
1Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu! 2#Yer 22:21; 5:3Hakuitii sauti; hakukubali kurudiwa; hakumwamini BWANA; hakumkaribia Mungu wake. 3Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; makadhi wake ni mbwa-mwitu wa jioni; hawasazi kitu cho chote hata siku ya pili. 4#Yer 23:11; Eze 22:26Manabii wake ni watu hafifu, wadanganyifu; makuhani wake wamepatia unajisi patakatifu, wameifanyia sheria udhalimu. 5#Kum 32:4; Zab 99:3,4BWANA kati yake ni mwenye haki; hatatenda uovu; kila asubuhi hudhihirisha hukumu yake, wala hakomi; bali mtu asiye haki hajui kuona haya. 6Nimekatilia mbali mataifa, buruji zao zina ukiwa; nimeziharibu njia kuu zao, hata hapana mmoja apitaye; miji yao imeangamizwa; hamna mtu hata mmoja, wala hapana akaaye huko. 7#Mwa 6:12Nalisema, Hakika utaniogopa, utakubali kurudiwa; ili yasikatiliwe mbali makao yake, sawasawa ya yote niliyoagiza katika habari zake; lakini waliondoka mapema na kuyaharibu matendo yao yote.
Adhabu na Wokovu wa Mataifa
8 # Mit 20:22; Yoe 3:2 Basi ningojeni, asema BWANA, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili nizikutanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu; kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu.
9Maana hapo ndipo nitakapowarudishia mataifa lugha iliyo safi, wapate kuliitia jina la BWANA, wamtumikie kwa nia moja. 10#Zab 68:31; Mal 1:11; Mdo 8:27Maana toka nchi iliyo mbali na mito ya Kushi, waniombao dua, yaani, binti za watu wangu waliotawanyika, wataleta matoleo yangu. 11#Mt 3:9Siku ile hutatahayarikia matendo yako yote uliyoniasi; maana hapo nitawaondoa watu wako wanaotakabari na kujivuna, wasiwe kati yako, wala hutatakabari tena katika mlima wangu mtakatifu. 12#Isa 14:32; 57:15; Mt 5:3; Lk 6:20Lakini nitasaza ndani yako watu walioonewa na maskini, nao watalitumainia jina la BWANA. 13#Ufu 14:5Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; wala ulimi wa hadaa hautaonekana kinywani mwao; kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewaogofya.
Wimbo wa Shangwe
14 # Zab 14:7 Imba, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee Israeli;
Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, Ee binti Yerusalemu.
15 # Yn 1:49; Eze 48:35; Ufu 21:3 BWANA ameziondoa hukumu zako,
Amemtupa nje adui yako;
Mfalme wa Israeli, naam, yeye BWANA, yu katikati yako;
Hutaogopa uovu tena.
16 # Isa 35:3 Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa,
Usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee.
17BWANA, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa;
Atakushangilia kwa furaha kuu,
Atakutuliza katika upendo wake,
Atakufurahia kwa kuimba.
18 # Omb 2:6 Nitawakusanya wanaousikitikia mkutano wa ibada, hao waliokuwa wa kwako; ambao mzigo uliokuwa juu yake ulikuwa fedheha kwao. 19Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya kuwa sifa na jina, hao ambao fedheha yao ilikuwa katika dunia yote. 20#Zab 22:27Wakati huo nitawaingizeni, na wakati huo nitawakusanya; kwa maana nitawafanya ninyi kuwa sifa na jina, miongoni mwa watu wote wa dunia, nitakapowarudisha wafungwa wenu mbele ya macho yenu, asema BWANA.

Currently Selected:

Sef 3: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy