YouVersion Logo
Search Icon

Zab 25

25
Sala ya Uongozi na Ukombozi
Zaburi ya Daudi.
1 # 1 Sam 1:15; Zab 86:4; Omb 3:41 Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu,
2 # Zab 7:1; 18:2; Rum 10:11 Ee Mungu wangu,
Nimekutumaini Wewe, nisiaibike,
Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.
3Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja;
Wataaibika watendao uhaini bila sababu.
4 # Kut 33:13; Zab 143:8; Mit 8:20 Ee BWANA, unijulishe njia zako,
Unifundishe mapito yako,
5Uniongoze katika kweli yako,
Na kunifundisha.
Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu,
Nakungoja Wewe mchana kutwa.
6Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako,
Maana zimekuwako tokea zamani.
7 # Zab 51:1 Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu,
Wala maasi yangu.
Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako,
Ee BWANA kwa ajili ya wema wako.
8BWANA yu mwema, mwenye adili,
Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.
9Wenye upole atawaongoza katika hukumu,
Wenye upole atawafundisha njia yake.
10Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli,
Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.
11 # Zab 31:3; 79:9; Rum 5:20 Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako,
Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi.
12 # Zab 37:23 Ni nani amchaye BWANA?
Atamfundisha katika njia anayoichagua.
13 # Zab 37:11,22,29 Nafsi yake itakaa hali ya kufanikiwa;
Wazao wake watairithi nchi.
14 # Mit 3:32; Yn 7:17; 2 Kor 4:2-6 Siri ya BWANA iko kwao wamchao,
Naye atawajulisha agano lake.
15 # Zab 141:8 Macho yangu humwelekea BWANA daima,
Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.
16 # Zab 69:16 Uniangalie na kunifadhili,
Maana mimi ni mkiwa na mteswa.
17Katika shida za moyo wangu unifanyie nafasi,
Na kunitoa katika dhiki zangu.
18 # 2 Sam 16:12 Utazame teso langu na taabu yangu;
Unisamehe dhambi zangu zote.
19Uwatazame adui zangu, maana ni wengi,
Wananichukia kwa machukio ya ukali.
20Unilinde nafsi yangu na kuniponya,
Nisiaibike, maana nakukimbilia Wewe.
21Ukamilifu na unyofu zinihifadhi,
Maana nakungoja Wewe.
22 # Zab 130:8 Ee Mungu, umkomboe Israeli,
Katika taabu zake zote.

Currently Selected:

Zab 25: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy