Mit 21:1-4
Mit 21:1-4 SUV
Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza po pote apendapo. Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo. Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka. Macho yenye kiburi, na moyo wa kutakabari, Hata ukulima wa waovu, ni dhambi.