YouVersion Logo
Search Icon

Mk 13

13
Kuharibiwa kwa Hekalu
1 # Mt 24:1-51; Lk 21:5-36 Hata alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, Mwalimu, tazama, yalivyo mawe na majengo haya! 2Yesu akajibu, akamwambia, Wayaona majengo haya makubwa? Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.
3Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, kuelekea hekalu Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea walimwuliza kwa faragha, 4Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya wakati, hayo yote yatakapokuwa karibu kutimia?
5Yesu akaanza kuwaambia, Jihadharini, mtu asiwadanganye. 6Wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye, nao watadanganya wengi. 7Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. 8#Isa 19:2; 2 Nya 15:6Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na matetemeko ya nchi mahali mahali; kutakuwako na njaa; hayo ndiyo mwanzo wa utungu.
Mateso Yajayo
9 # Mt 10:17-20; Lk 12:11-12 Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao. 10#Mk 16:15Na sharti Injili ihubiriwe kwanza katika mataifa yote. 11Na watakapowachukua ninyi, na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu. 12#Mik 7:6Na ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, na baba atamsaliti mtoto, na watoto watashambulia wazazi wao, na kuwafisha. 13#Mt 10:22; Yn 15:21Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Chukizo la Uharibifu
14 # Dan 9:27; 11:31; 12:11 Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; 15#Lk 17:31na mtu aliye juu ya dari asishuke, wala asiingie kuchukua kitu nyumbani mwake; 16naye aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake. 17Lakini ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku hizo! 18Ila ombeni yasitokee hayo wakati wa baridi. 19#Dan 12:1; Mdo 7:14; Yoe 2:2Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe. 20Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo. 21Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki; 22#Kum 13:1kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule. 23Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele.
Kuja kwa Mwana wa Adamu
24 # Isa 13:10; Eze 32:7; Yoe 2:10,31; 3:15; Ufu 6:12 Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake. 25#Isa 34:4; Yoe 2:10; Mdo 6:13na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. 26#Dan 7:13; Ufu 1:7Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. 27#Zek 2:6; Kum 30:4; Mt 13:41Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu.
Funzo la Mtini
28Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu; 29nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni. 30Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie. 31Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Haja ya Kuwa Waangalifu
32 # Mt 24:36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
33Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. 34#Lk 12:36-38; 19:12; Mt 25:14Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe. 35#Lk 12:38Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; 36asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. 37Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.

Currently Selected:

Mk 13: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy