YouVersion Logo
Search Icon

Mik 5

5
Mtawala kutoka Bethlehemu
1 # Ayu 16:10; Omb 3:30; Mt 27:30 Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
2 # Mwa 35:19; 49:10; Zab 132:6; Isa 9:6; Zab 90:2; Mit 8:22; Yn 1:1; Mt 2:6; Yn 7:42 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele. 3Kwa sababu hiyo atawatoa, hata wakati wa kuzaa kwake aliye na utungu; ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia wana wa Israeli. 4#Zab 72:8; Isa 52:13; Zek 9:10; Lk 1:32Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za BWANA, kwa enzi ya jina la BWANA, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hata miisho ya dunia. 5#Isa 9:6; Lk 2:14; Efe 2:14; Kol 1:20Na mtu huyu atakuwa amani yetu; wakati Mwashuri atakapoingia katika nchi yetu, na kuyakanyaga majumba yetu, hapo mtaondokesha wachungaji saba juu yake, na wakuu wanane. 6#Lk 1:71; Mwa 10:8-11Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake; naye atatuokoa na Mwashuri, atakapoingia katika nchi yetu, na kukanyaga ndani ya mipaka yetu.
Wajibu wa Mabaki
7 # Zab 110:3 Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa BWANA, mfano wa manyunyu katika manyasi; yasiyomngojea mtu, wala kuwakawilia wanadamu. 8Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa, kati ya kabila nyingi, mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwana-simba kati ya makundi ya kondoo, ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyaga-kanyaga na kurarua-rarua, wala hakuna wa kuokoa. 9Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali.
10 # Zek 9:10 Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema BWANA, nitawakatilia mbali farasi zako watoke kati yako, nami nitayaharibu magari yako ya vita; 11nami nitaikatilia mbali miji ya nchi yako, na ngome zako zote nitaziangusha; 12nami nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako; wala hutakuwa tena na watu wenye kutabana; 13#Zek 13:2; Isa 2:8nami nitakatilia mbali sanamu zako na nguzo zako, zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako. 14Nami nitayang’oa maashera yenu, yasiwe kati yako; nami nitaiangamiza miji yako. 15Nami nitajilipiza kisasi katika hasira na ghadhabu juu ya mataifa wasiosikiliza.

Currently Selected:

Mik 5: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy