YouVersion Logo
Search Icon

Mt 7

7
Kuwahukumu Wengine
1 # Rum 2:1; 1 Kor 4:5 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. 2#Mk 4:24Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. 3Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? 4Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? 5Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Kutweza Kitakatifu
6 # Mt 10:11 Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Omba, Tafuta, Bisha
7 # Mk 11:24; Lk 11:9-13; Yer 29:13,14; Yn 14:13; 16:23 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; 8kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. 9Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? 10Au akiomba samaki, atampa nyoka? 11#Yak 1:17Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Amri Kuu
12 # Lk 6:31; Mt 22:39,40; Rum 13:8-10 Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.
Mlango Mwembamba
13 # Lk 13:24; Yn 10:7,9 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. 14#Mt 19:24; Mdo 14:22Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Mti na Matunda Yake
15 # Mt 24:4,5,24; Mdo 20:29 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. 16#Gal 5:19-22; Yak 3:12Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17#Mt 12:33Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. 18Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. 19#Mt 3:10; Lk 3:9; Yn 15:2,6Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 20#Mt 12:33Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.
Kuhusu Wanaojihadaa
21 # Mt 21:29; Rum 2:13; Yak 1:22,25; 2:14; 1 Kor 12:3 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22#Yer 14:14; 27:15; Lk 13:25-27; 1 Kor 13:1,2Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23#Zab 6:9; Mt 13:41; 25:41; 2 Tim 2:19Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Wasikiao na Watendao
24 # Mt 7:21 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; 27#Eze 13:10,11mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
28 # Mk 1:22; Lk 4:32; Mt 11:1; 13:53; 19:1; 26:1 Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; 29#Yn 7:46kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.

Currently Selected:

Mt 7: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy