YouVersion Logo
Search Icon

Mt 23

23
Yesu Awakana Waandishi na Mafarisayo
1 # Mk 12:38-40; Lk 20:45-47; Lk 11:39-52 Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema, 2Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; 3#Mal 2:7,8basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi. 4Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. 5#Mt 6:1; Hes 15:38; Kum 6:8; Kut 13:9Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao; 6#Lk 14:7; Mt 6:5hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, 7na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi. 8Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu.
9Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. 10Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. 11#Mt 20:26-27; Mk 9:35; 10:43-44; Lk 22:26Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. 12#Lk 14:11; 18:14; Mit 29:23; Ayu 22:29; Eze 21:26; 1 Pet 5:5Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa.
13Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.
14[Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.]
15Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.
16 # Mt 15:14 Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amejifunga. 17Wapumbavu ninyi na vipofu; maana ni ipi iliyo kubwa, ile dhahabu, au lile hekalu liitakasalo dhahabu? 18Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga. 19#Kut 29:37Vipofu ninyi; maana ni ipi iliyo kubwa, ile sadaka, au ile madhabahu iitakasayo sadaka? 20Basi yeye aapaye kwa madhabahu, huapa kwa hiyo, na kwa vitu vyote vilivyo juu yake. 21Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo, na kwa yeye akaaye ndani yake. 22#Isa 66:1; Mt 5:34Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa yeye aketiye juu yake.
23 # Law 27:30; Mik 6:8 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. 24Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.
25 # Mk 7:4 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi. 26#Tit 1:15; Yn 9:40Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi.
27 # Mdo 23:3 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. 28#Lk 16:15Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi.
29Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, 30na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii. 31#Mdo 7:52Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii. 32Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. 33#Mt 3:7; 12:34; Lk 3:7Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? 34#Mt 13:52; 10:23; 1 The 2:15Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji; 35#Mwa 4:8; 2 Nya 24:20-21hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu. 36Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.
Maombolezo juu ya Yerusalemu
37 # Lk 13:34,35; Mdo 7:59; 1 The 2:15 Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka! 38#Yer 22:5; 12:7; 1 Fal 9:7,8Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa. 39#Zab 118:26; Mt 21:9Kwa maana nawaambia, Hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.

Currently Selected:

Mt 23: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy