YouVersion Logo
Search Icon

Mt 17

17
Kugeuka Sura
1 # 2 Pet 1:17-18 Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani; 2#2 Pet 1:16-18akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. 3Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye. 4Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. 5#Mwa 22:2; Kum 18:15; Zab 2:7; Isa 42:1; Mt 3:17; 12:18; Mk 1:11; Lk 3:22Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye. 6Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana. 7Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope. 8Wakainua macho yao, wasione mtu ila Yesu peke yake.
9 # Mt 16:20 Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu. 10#Mal 4:5; Mt 11:14Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? 11Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, 12#Mt 11:14; 14:9,10ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao. 13#Lk 1:17Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.
Yesu Aponya Mvulana Mwenye Pepo
14 # Mk 9:14-29; Lk 9:37-42 Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, 15Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. 16Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya. 17#Kum 32:5; Yn 14:9Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. 18Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. 19#Mt 10:1Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 20#Mt 21:21; Mk 11:23; 1 Kor 13:2; Lk 17:6Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. 21[Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]
Yesu asema tena juu ya Kufa na Kufufuka kwake
22 # Mk 9:30-32; Lk 9:43-45 # Mt 16:21 Nao walipokuwa wakikaa Galilaya, Yesu akawaambia, Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua, na siku ya tatu atafufuka. 23Wakasikitika sana.
Yesu na Ushuru wa Hekalu
24 # Kut 30:13; 38:26 Hata walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli? Akasema, Hutoa. 25Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni? 26Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru. 27Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli#17:27 Shekeli moja ni kama shilingi 3.; ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.

Currently Selected:

Mt 17: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy