Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani
Read Lk 4
Share
akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.
Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate.
Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.
Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.
Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.
Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini
kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde
na ya kwamba, Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda.
Compare All Versions: Lk 4:1, 2, 3, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12, 13
Save verses, read offline, watch teaching clips, and more!
YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy
Home
Bible
Plans
Videos